Decoration & Catering Services

Decoration & Catering Services

Boutique

Boutique

Tuesday, February 25, 2014

Duh! Kumbe JB ni Mr misifa?

JB

Kama ni mfuatiliaji wa movie za Kibongo, basi jina na sura hii si ngeni machoni pako, ambapo msanii huyu ni mmoja kati ya wasanii wanaojulikana sana hapa nchini.

Watu wengi humpenda msanii huyu ambae ni mwenyeji wa Kilimanjaro kwa jinsi alivyo mahiri katika uigizaji wake, na huku wengine wakisema kuwa umaarufu wake umeongezeka baada tu ya kifo cha Marehemu Stephen Kanumba.

Sasa usichokijua kwa Bwana kaka huyu ni kwamba, katika wasanii wa Kitanzania wanajulikana sana na wanaopenda sifa na maringo, yeye ni mmoja wao, ambapo kwa mara kadhaa amekuwa akikutwa na waandishi wetu katika hali hiyo ya kujisikia na kupenda hizo zinazojulikana kuwa nisifa.

Kituko cha mwisho ambacho kilidhihirisha jambo hilo, ni katika msiba wa msanii mmoja wa kundi la Jakaya Theatre (mwanamama), aliyefariki hivi majuzi, ambapo naye alihudhuria na kuonekana akizurura sana kwa madaha huku akiwaangalia angalia watu, kana kwamba anahitaji wamuone, jambo ambalo vijana na kila aliyemtazama Msanii huyo, ambaye kwa siku hiyo alivalia shati nyeusi na miwani kubwaaaa, aliona kuwa ni mauzo.

Mashabiki na marafikize, Je, ni kweli JB ni misifa?

0 comments:

Post a Comment