Decoration & Catering Services

Decoration & Catering Services

Boutique

Boutique

Monday, November 19, 2012

MUME WA HAYATI ANGELA CHIBALONZA AJALIWA MTOTO WA KIUME KATIKA NDOA YAKE MPYA

 Dantsan Bill Canaan mtoto wa pastor Elisha Muliri akiwa amebebwa na mama yake.
Mchungaji kiongozi wa huduma ya Shekinah International yenye makao makuu yake jijini Nairobi nchini Kenya Pastor Elisha Muliri ambaye ni mume wa aliyekuwa kipenzi cha wengi katika medani ya muziki wa gospel afrika mashariki na kati na nje ya bara la Afrika hayati Angela Chibalonza. Mungu amembariki kwa zawadi ya mtoto wa kiume katika ndoa yake mpya na mkewe kipenzi Maguy (Magret).
Katika mawasiliano na Gospel Kitaa, Pastor Muliri ambaye alikuwa nchini Afrika ya kusini hivi karibuni kwa huduma, amesema anamshukuru Mungu kwa zawadi hiyo ya mtoto wa kiume waliyempa jina la Dantsan Bill Canaan kama alivyoliandika jina la mwanaye huyo wakati wa mawasiliano na GK, ambapo kwasasa familia yake ina jumla ya watoto 4 ukiongeza na watoto 3 waliopewa na Mungu akiwa na marehemu mkewe Angela Chibalonza.
Ni miaka 5 sasa tangu kufariki kwa Angela Chibalonza, ambaye alifariki kwa ajali ya gari akiwa na mwimbaji wake mmoja Nimrodi Makori pamoja na dereva wake Kennedy Aluoch mnamo tarehe 22, September 2007 zikiwa zimebakia siku nane kabla hajazindua album yake ya mwisho ''Nimekutana na Yesu'' ambayo hata hivyo ilizinduliwa kama ilivyopangwa kwa waimbaji mbalimbali kutoka Tanzania, Kenya na Congo ikiwa kama kumuenzi na kumshukuru Mungu kwa utumishi wa Angela duniani, kabla hajasafirishwa kwa mazishi nyumbani kwao Bukavu huko nchini Congo.
Kuna waimbaji wengi ambao wamenufaika kuwa chini ya Angela enzi za uhai wake akiwemo wmimbaji nyota wa sasa bwana Solomon Mukubwa na wengineo ambao walikuwa katika band ya Angela kama waitikiaji wake.

0 comments:

Post a Comment