Decoration & Catering Services

Decoration & Catering Services

Boutique

Boutique

Thursday, October 2, 2014

Itazame viedo kali yake Rich Mavoko Pacha wangu

Rich Mavoko


Thursday, September 11, 2014

Friday, September 5, 2014

Exclusive: Sasa waweza pata habari zote za burudani za kiinjili kupitia Gospeltz.com

Ni mtandao wa kwanza hapa nchini kuweza kufunguliwa kwa lengo moja tu la kutoa burudani kwa wapenzi wa nyimbo za Injili huku ikiwapa fursa ya kuwajua wasanii wa aina hiyo ya muziki, maisha yao kwa kina na mapana, huku ikitoa nafasi kwa wasanii hao kutambulisha nyimbo zao kila siku.

Mtandao huo ambao kwasasa tayari una page saidizi Facebook, inayokwenda kwa jina la GospelTz, huku website yenyewe ikitumia domain hii; www.gospeltz.com, utakuwa ukiendeshwa kwa masaa 24 na kwa ufanisi wa hali ya juu, huku habari zake zote zikiwa ni za uhakika kwa asilimia zote.

Chakufanya ni kwenda kwenye account yako ya facebook, kisha tafuta page hii GospelTz, 'Like', kisha hamia kwenye website yenyewe ambayo ni www.gospeltz.com upate habari za kutosha za viwango vya hali ya juu.

Wednesday, August 27, 2014

COMING SOON!!!!


Yule msanii wa nyimbo za Injili hapa nchini aliye tamba na vibao vyake viwili 'Tumekuja kuzungumza na wewe' pamoja na ' Bwana tunakutukuza",Gadiel Mpungu,  hivi sasa yupo mbioni kuachia yimbo yake mpya iitwayo Nalingi Yo Mingi Yesu, ikiwa na maana ya Nakupenda sana Yesu. Ni lini ataiachia,ameirekodi wapi, na kwanini akachanganya lugha, yote ataeleza hapa hapa hivi karibuni.  Stay tuned

Sunday, August 10, 2014

Mumewe Mbasha atelekeza hata marafiki wa karibu.


Mume halali wa mwanamuziki wa muziki wa Injili hapa nchini Flora Mbasha, ndugu Emmanuel Mbasha, kwasasa inaelezwa kuwa amejitenga kabisa na marafikize waliyokuwa karibu kipindi cha mwanzo.

Hayo yameelezwa leo na mmoja kati ya waliyowahi kuwa washambulia jukwaa wake, huku akionyesha hali ya kusikitishwa sana na kitendo hicho pamoja na kumuonea huruma.

"yaani kaka ninavyo ongea na wewe, nina kama mwaka sasa sijaonana na bro Emmanuel Mbasha, na tangu litokee hili sakata lake la juzi, ndo kabisa hata nikimpigia simu au kumtumia msg japo nimtie moyo kama mdogo wake aliye nikuza katika tasnia, hata hapokei" alisema kijana huyo (jina limehifadhiwa).

Aidha kijana huyo pia aliongeza kuwa katika sakata hili la Mbasha na Mkewe, "jazba" zao zinaweza zikawa ni chanzo kikubwa cha wao kufika hapo walipofika, kwani kuna wakati walikuwa wakigombana kwa vitu vidogo sana kitu ambacho kama mmoja kati ya wawili hao hakuwa na akili iliyo tulia, basi angeweza fanya maamuzi ya ajabu kama haya ya sasa, yaliyo idhalilisha tasnia ya muziki wa Injili hapa nchini.

Emmanuel Mbasha na mkewe Flora, walingia kwenye mgogoro mkubwa wa ndoa, ambapo Emmanuel alishukiwa kumbaka mdogo wa mwanadada huyu aliyewahi tamba na kibao chake cha " Jipe moyo", huku Emmanuel akikanusha madai hayo kwa kusema kuwa ni njama zilizo tengenezwa ili kuwatenganisha kwani kwasasa mkewe ana mahusiano na kiongozi mmoja wa kiroho hapa nchini.

Marekani kuendelea kuishambulia Iraq.


Marekani imeendeleza mashambulizi ya anga kaskazini mwa Iraq kwa lengo la kuwasaidia Wakrud katika mji wa Erbil dhidi ya wapiganaji wa kiislam wa kundi la Jihad.
Wapiganaji wa kundi hilo la Kiislam hivi karibuni wameendelea kuimarisha ngome yao katika eneo hilo ikiwa ni pamoja na kuiteka ngome kubwa ya Iraq katika mji wa Mosul.
Jeshi la Marekani limesema limefanya mashambulizi dhidi ya wapiganaji wa Sunni waliokuwa wamejificha katika milima iliyo eneo la wakimbizi la Yazid.
Hata hivyo Uingereza imesema inaendelea kutoa misaada ya kibinadamu kwa Wakurdi ambapo Ofisa wa zamani wa mambo ya kigeni wa Uingereza Alistair Burt anasema nchi hiyo inaweza kusaidia eshi la Wakurdi.
Wakati huo huo vikosi vya majeshi ya Iraq na vyombo vya usalama vimesambaa katika katika maeneo mbalimbali ya mji wa Baghdad huku kukiwa na hali ya wasiwasi kufuatia kauli iliyotolewa na waziri mkuu wa nchi hiyo ya Iraq Nouri al-Maliki inayodaiwa kuwa ni ya utovu wa nidhamu kwa Rais wa nchi hiyo Fuad Masum.
Amesema kuwa Rais wa Jamhuri hiyo amevunja katiba mara mbili,mara ya kwanza ni pale alipojiongezea muda wa kukaa madarakani,wakati alistahili kutangaza kuvunja bunge. Hata hivyo kipindi chake kiliisha august saba alhamisi iliyopopita.
Hata hivyo papa Francis ameelezea gogoro wa Ira kwamba msingi wake mkubwa ni masuala ya tofauti za kidini. Melfu ya watu nchini Iraq wamekuwa wakilazimishwa na wapiganaji wa kiislam ambao wameimarisha ngome ao kaskazini mwa nchi hiyo.Katika ujumbe wake wa jumapili ,papa Francis ametoa wito kwa dunia kukomesha uhalifu huo unaoendelea nchini Iraq.

Chanzo: BBC swahili

Monday, August 4, 2014

Photo of the day

Designer and model Veronica Lugenzi

"Mzee wa Upako" Antony Lusekelo akiri wazi kuwa yeye si nabii.

Mchungaji mkuu wa kanisa la GRC Ubungo Kibangu, Antony Lusekelo alimaarufu kama Mzee wa Upako, akiri hadharani kuwa yeye si Nabii bali ni Baba Mchungaji.

Mzee wa Upako aliyasema hayo jana katika ibada ya Jumapili alipokuwa akieleza jinsi anavyo kerwa na tabia za baadhi ya watumishi kujipa majina makubwa kuliko kazi wanazo zifanya.

Aidha Mzee wa Upako alisisitiza kuwa, kama mtumishi wa Mungu hupaswi kujitetea na kujikinga kwenye majina makubwa na badala yake kufanya kazi ya Mungu kwa uaminifu na kisha matunda ya kazi yako ndo yaeleze wazi kuwa wewe ni nani.

Kwasasa mtumishi huyu wa Mungu mwenye umahiri wa kuhubiri ipasavyo, ndiye mwenye kibali kikubwa hapa nchini tangu kwa watoto, vijana, watu wazima na hata viongozi wa nchi.

Medical service providers get training on ICT


At least 72 Marie Stopes health workers from several centres across the country have received information and Communication Technology (ICT)training  to help them better adopt modern technological systems and methodologies.
 
Offered by the College of Business Education (CBE) the training is part of ongoing efforts to improve health services in the country explains the CBE Training Coordinator Ogakhan Nyamu, he also noted that the training will facilitate their access to health information across the world.
 
Speaking at the end of the ICT training over the weekend in Dar es Salaam, he said the training has enhanced the health workers’ capacity to manage global health challenges which need technological solutions.
 
“There are many challenges in the health sector, some of which can be solved using modern information and communication technologies,” said Nyamu, who was also an ICT lecturer at the CBE.
 
Another ICT lecturer from CBE, Godfrey Mwandosya, said the training was conducted to improve the provision of medical services through access to modern technology.
 
“The ICT training will speed up service provision and ease access to information,” he explained.
 
Commenting, the Marie Stopes Country Director, Ulla Muller, said the five-day training has increased workers’ confidence in the use of ICT and will have positive impacts on the health sector.
 
She urged the trainees to share the knowledge with other staff and seek further learning opportunities to better their performance capacity
Dr. Peter Mwampambe, also from Marie Stopes, said new knowledge is essential to improvement of health service delivery and reduction of mortality rate in the country. 
 
He said lack of ICT education is among the main challenges facing health workers, especially in Tanzania’s rural areas.
 
He said the training offered by CBE will help develop ICT skills for the effective handling of the health sector’s technical issues and pledged that CBE will continue to provide similar trainings to medical institutions across the country. 

Thursday, May 29, 2014

Uchungaji wa Flora Mbasha, wamfanya mumewe Emannuel abake

Wakati kesi ya ubakaji inayo mkabili mume wa mwanamuziki wa nyimbo za Injili hapa nchini, Emmanue Mbasha, lawama sasa zaelekezwa kwa Flora Mbasha ambae ndiye mke mtu.
Lawama hizo zimetolewa na  baadhi ya watu waliyo karibu sana na familia hiyo, kuwa mwanamama Flora Mbasha, ambae kwasasa yuko katika mafunzo na mbioni atakuwa mchungaji wa kanisa fulani hapa mjini, humuacha sana mume wake, kutokana na wingi wa safari za kimafunzo alizo nazo Flora jambo ambalo linatathiminiwa kuwa gumu kwa mwanamume yoyote yule, licha ya kuonekana kuwa chanzo cha Emanuel Mbasha kumbaka shemejie.
Mpaka sasa Emamnuel Mbasha haijajulikana yupo wapi, japo tayari ameshafunguliwa kesi  yenye Kumbukumbu Na. TBT/RB/3191/2014 na ya Jalada  la  Uchunguzi  Na. TBT/IR/1865/2014

Mamia wamlilia 'Maxmilian Ngobe'.

Gari ya maiti ilipofika Uwanjani Leaders Club


Ndipo ndugu, jamaa na marafiki walipoanza kuubeba mwili wa rafiki yao Maxcmilian Ndube.




Aliyebeba msalaba ni moja kati ya vijana waliyo kuwa wakifanya kazi na marehemu pale Mliimani Tv, na wa nyuma mwenye picha ndiye mtoto wake wa kwanza.

Mamia ya watu walihudhuria

Mwakilishi wa waandishi wa habari.

 mwakilishi wa madereva bajaji Makubusho, Bw. Chaurembo akizungumza kwa niaba ya madereva bajaji wa kituo cha Makumbusho, ambao walikuwa marafiki wakubwa wa marehemu.

Shamimu Mlacha, Zainabu Mtima na Khadija Mzee katika hali ya taharuki na majonzi tele wakiwa kama wafanyakazi wenzie na marehemu Max, pale Mlimani Tv.

Dkt. Warioba akiuaga mwili wa marehemu.

 Jerry Muro nae alitoa heshima zake za mwisho

Mkongwe wa tasnia ya habari, Ernest Mrutu, amabe pia alikuwa ni mfanyakazi mwenzie na marehemu, akitoa heshima zake za mwisho.

Hivi ndivyo ilivyokuwa jana pale leaders Club, katika msiba wa Maxmilian Ngobe, aliyezaliwa mwaka 1960 kule nchini Congo na kufikwa na umauti kwasababu na maradhi ya ini, pamoja na moyo kuwa mkubwa.

Mpaka umauti unamfika, marehemu Maxmilan alikuwa ni mpiga picha wa Mlimani Tv, kituo kilichopo chini ya chuo kikuu cha Dar es Salaam, akitokea katika gazeti na Star Tv, alikowahi kufanya kazi kwa miaka mitano mfululizo.

Marehemu Maxmilani Ngobe ameacha mjane, watoto wakiume watatu na wakike mmoja ambao k

Tuesday, May 27, 2014

'RECHO HAULE' amfuata 'Adam Kuambiana'

Baada ya kifo kilicho washitua wengi hapa nchini, kifo cha msanii na Director mahiri ' Adam Kuambiana', leo habari zilizotufikia, ni kwamba mwanadada Recho Haule nae ametutoka duniani.

Kifo hiki kilichotokea leo asubuhi, inasemekana kuwa kilitokea wakati mwanadada huyu alipokuwa akijifungua mtoto wake wa pili.

Tutazidi kukuhabarisha mengi juu ya msiba huu. Mungu amuweke mahala pema peponi!