Decoration & Catering Services

Decoration & Catering Services

Boutique

Boutique

Saturday, March 1, 2014

Masikini Mziwanda, naye anasa kwenye tundu bovu la Shilole.

Nuh Mziwanda akitumbuiza Otea nani, kibao kinachofanya vyema nchini.


Hatimaye msanii chipukizi, Nuh Mziwanda Chachalundoa sasa naye anasa kwenye tundu bovu la kuwa na mahusiano na mwanadada anayekiri kila leo, kuwa anakomaa na Jiji na hatorudi Igunga, Zuwena Mohammed a.k.a Shilole.

      
     Nuh akiwa na Shilole katika pozi

Habari hizo zenye ukweli ndani yake, tulizipata toka kwa msanii mmoja maarufu sana hapa nchini, aliyekuwa akilielezea hili kwa masikitiko makubwa na akionyesha dhahiri kumuonea huruma kijana huyu anayechipukia kwenye tasnia hii ya muziki wa Bongo Fleva, kwa kusema kuwa mahusiano ya Nuh na Shilole, hayaundwi na mapenzi, bali yanaundwa na tabia ya vijana wengi wa kileo, ya kupenda umaarufu aliyouita wa kijinga na kupenda mteremko katika maisha.

'Unajua ndugu yangu wacha nikuambie, hawa vijana wanaochipukia kwenye game wanakuwa kama wanaulimbukeni fulani. Yani wengi kati yao hudhani kutoka ni mpaka utembee na staa ndo jamii itakuelewa au labda mpaka upate maskendo skendo, ndo itakuwa gia yako ya kutokea, kitu ambacho sicho.  Sasa ndicho alichoingia mkenge huyu dogo anae jiita last born ( Nuh), kila siku ana kazi ya kushinda na kulala kwa Shilole, as if amemuoa hivi, pasipo kufikiria hata kuwa hivyo vijipesa na huo umaarufu wa huyo Shishi Babe ameupataje' alisema Msanii huyo huku akionyesha kutofurahishwa kabisa na kitendo hicho.


         
     Shilole

Akiendelea kutupa nyepesi nyepesi hizo, msanii huyo aliongeza kuwa, haipendi kabisa tabia ya mwanadada huyo kutoka Igunga, kwani licha ya kuwa na dogodogo kama Nuh, Young Killer na wengineo, CV yake ya hapo kitambo kabla ya kuwa Shilole huyu tunayemjua, ilikuwa ni chafu, na kama ingetolewa maksi, basi angepata miswaki ya kutosha ( F).

Fiesta Super Nyota 2012, Young Killer

Aidha hatukutaka kuyaamini moja kwa moja maneno ya msanii huyo aliyetupa habari, na ndipo ilipotulazimu kuwasiliana na Mziwanda ambapo mazungumzo yetu yalikuwa hivi;

Mwandishi: Nuh, mambo vipi?

Nuh: Fresh tu.

Mwandishi: Hivi ni kweli unatoka na Shilole?

Nuh: We nan?

Mwandishi: Mimi ni ..........?!>?

Nuh: Kwan sipasw kuwa nae?

Mwandishi: (baada ya kulielewa jibu lile, kiutuuzima) Poa poa kaka.

Nuh: Yeah men.



Aidha kwa upande wa shilingi wa uvumi huu, yaani kwa mwanadada ambaye kihistoria alishawahi kubakwa akiwa na miaka 16, yeye anaonyesha wazi kuridhishwa na kuwa huru kwa kuwa na mahusiano na Serengeti Boys, hususani wanaochipukia kwenye muziki huu wa Bongo Fleva, kwani katika moja ya majibu yake katika swali aliloulizwa na mtandao mmoja hapa nchini (jina tumeliihifadhi kwa maslahi binafsi), juu ya tabia yake hiyo, alisikika akijibu hivi;

“Ninavyojua mapenzi hayachagui umri mkubwa wala mdogo, nawashangaa hao wanaosema hivyo, sasa wanataka niwe na wazee? Mimi ni kijana, lazima niwe na uhusiano na vijana wenzangu.”

Hivyo ni dhahiri kuwa wasanii hawa wanamahusiano, ambapo kwa upande wa Nuh, huwenda akawa ameamua kutoa majibu ya nyimbo yake ya Otea nani, kuwa Shilole ndiye yule msichana mzuri asiye na kifani aliye muimba.

0 comments:

Post a Comment