Mwanamuzi mashuhuri nchini kongo(DRC) Anton Akgeba Makila Mabe maarufu pia kama Koffi Olomide aka Mopao Mokonzi, Aswekwa lupango na pia kafikishwa kwa Pilato
Mwanamuziki huyo alikamatwa na kufungiwa
katika kituo cha polisi na kufikishwa mahakamani jumatano.
Koffi alikamatwa kufuatia vurugu katika
hoteli moja mjini Kinshasa.
Waandishi wa habari wanasema mahakama
hiyo ya Kinishasa ilifurika kutokana na watu wengi kuja kumuona
kiongozi huyo wa bendi ya Quartier Latin akiwa kizimbani.
Kesi hiyo iliharishwa hadi Alhamisi
asubuhi wakati atakaposhitakiwa rasmi.
Wakati wa kesi hiyo hapo jana Koffi
Olomide aliwakilishwa na mawakili 10.
Ugomvi kati ya mwanamuziki huyo na
mtayarishi wake Bwana , Diego Lubaki, ni kuhusu pesa dola $3,680.
Hakimu alimfahamisha mwanamuziki huyo
ikiwa atapatikana na hatia huenda akafungwa jela miezi sita.
Olomide ni gwiji wa muziki aina ya
"soukous", mtindo ulitokana na jina la kifaransa "secouer", lenye maana
ya kujitikisa au kujinengua ,na wachezaji wake vile vile wanatambulika
kwa kunengua maungo.
0 comments:
Post a Comment