Mwimbaji wa muziki wa Injili nchini, Miriam Lukindo Mauki ‘Binti
Afrika’ Jumamosi hii anatarajiwa kuiteka Matembele ya Pili, Ukonga
jijini Dar es Salaam atakaposhiriki uzinduzi wa albamu mbili za kwaya ya
Sauti za Sifa iliyo chini ya Huduma ya The Word of Reconciliation
Ministries (WRM).
Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Mwalimu wa kwaya hiyo,
Elibariki Isango, alisema, Miriam amekubali kuungana nao na siku hiyo
atapanda jukwaa moja na Christina Shusho kuimba, wakati wa uzinduzi wa
albamu zao hizo ambazo ni ‘Enendeni kwa Roho’ na ‘Pokea Sifa’.
0 comments:
Post a Comment