Mustafa
Hassanali aalikwa kwenye Maonesho ya color in
the Desert.
“Pink Desert
Collection Toleo la nne la” Hassanali’ mwaka 2012
Mustafa
Hassanali kuhamasisha juu ya kansa ya maziwa kupitia mitindo.
Mwanamitindo mkongwe ndani ya Afrika
anayetokea Tanzania Mustafa Hassanali amealikwa katika maonesho ya
mitindo ya color in the desert yanayofanyika kuanzia tarehe 31 agost
hadi tarehe 1 septemba ikiwa ni mara ya pili kufanyika nchini Botswana katika mji mkuu wa Gaborone.
Akiwa ni
mtanzania pekee aliyealikwa katika maonesho hayo ya mavazi yanayosifika
Botswana
na Afrika
kwa ujumla Hassanali anasema “ Nimefurahi sana na anajisikia fahari na
heshima
kuzindua toleo langu jipya la mtindo ikiwa ni la nne ndani ya
mwaka huu na nategemea kutumia
fursa hii kuutangaza utamaduni wetu na
kuboresha urafiki uliopo kati ya Botswana na Tanzania”.
Toleo hili linaloitwa
Pink Desert collection lina magauni yenye alama ya Mustafa Hassanali ikiwa ni pamoja na nguo za kiume ambazo ziko tayari
kwa kuvaliwa na kuonesha umaridadi wa mbunifu huyo.
Toleo hili linatoka na kuzinduliwa ikiwa ni
kipindi tunachoelekea mwezi oktoba ambao unajulikana duniani kote kuwa
ni mwezi wa kuhamasishana dhidi ya ugonjwa wa kansa ya matiti.
‘”Nitatumia
toleo hili la mitindo pia katika kuhamasisha na kuelimisha jamii
kuhusiana na tatizo la ugonjwa wa kansa ya matiti ili kila mwanamke
aweze kuwa na uelewa wa kujichunguza mwenyewe juu ya afya yake,
sambamba na kupenda kuvaa nguo zenye rangi ya pinki kama kiashiria cha
uelewa juu ya kansa ya matiti ugonjwa ambao unaathiri wanawake wengi.”
Alimalizia Mustafa Hassanali.
Kwa mwaka 2012 Mustafa Hassanali ameshazindua
matoleo matatu ya mavazi ambayo ni, Afrikalos aliyoonesha Nchini
Nigeria (Lagos), Toleo la Harusi aliloonesha Tanzania (Dar es salaam) na
toleo maalumu la mwezi wa Ramadhani liliooneshwa Dakar Senegal.
0 comments:
Post a Comment