Decoration & Catering Services

Decoration & Catering Services

Boutique

Boutique

Sunday, January 6, 2013

FLORA MBASHA ABARIKI WATANZANIA LONDON, WAMPA MWALIKO MWINGINE APRIL

 Flora Mbasha akiwa kazini.

Emannuel na Flora Mbasha katika pozi ibadani hapo.
 
Hivi karibuni ilikuwa ni siku ya kipekee kwa Watanzania waishio jijini London nchini Uingereza baada ya kupata wasaa mzuri wa kumsifu Mungu wakiongozwa na nyota wa gospel Tanzania Flora na mumewe Emanuel Mbasha ambao wapo nchini humo kwa ziara ya kihuduma.

Waimbaji hao walianza huduma yao katika kanisa la Vision Gospel Ministries lililopo maeneo ya Hackney Wick chini ya askofu Ernest Irungu ambaye aliweza kubariki waumini waliohudhuria ibada hiyo kwa neno zuri kwamba mwaka huu ni mwaka ambao Mungu anakwenda kufanya maisha yao kwa upya, lakini wanatakiwa wawe watu wa Maombi, Msamaha huku mkalimani wake Dkt. Monica Mhoja kutoka Scotland ambaye ndiye aliyefanikisha ujio wa waimbaji hao,aliwavutia waumini hao kwa ukalimani wake maridadi wa lugha ya kiswahili.

Lakini kama hiyo haitoshi baraka ya uimbaji kutoka kwa Flora na mumewe iliwafanya waumini hao kutotulia vitini na kuamua kusifu na kucheza pamoja na waimbaji hao hadi mwisho wa uimbaji hali ambayo ilifanya hata wakati walipomaliza uimbaji tayari kuondoka kuelekea kanisa jingine baadhi ya waumini hao walitaka waimbaji hao waendelee hata hivyo haikuwezekana na kuamua kuwaunga mkono waimbaji hao kwakununua CD's na DVD zao.

Aidha baada ya kutoka hapo waimbaji hao walishiriki katika ibada nyingine inayowajumuisha watanzania  inayofanyika katika kanisa la The William Temple lililopo eneo la Enysham Drive Abbeywood, London ambako ibada zao huanza mchana chini ya mtume Mathew Jutta, ambako huko waimbaji hao waliachiwa mda mrefu wa kuimba na kubariki wengi kwani kama ilivyokuwa katika kanisa la awali waumini hawakutaka waimbaji hao kumaliza ikabidi wapewe upendeleo wa kuimbiwa wimbo mmoja zaidi mwishowe waliwabariki waimbaji hao kwakununua CD'S zipatazo sita kwa paundi 400 ambazo ni sawa na shilingi milioni moja za kitanzania.

Kwa pamoja Watanzania wanchini Uingereza wamewaomba waimbaji hao kurejea tena nchini humo mwezi wa nne mwaka huu kwa huduma zaidi kwakuwa wakati huu wengi wao walirudi nyumbani kwa ajili ya sikukuu, ambapo waimbaji hao wamekubali mwaliko huo nakuwataka waumini hao waendelee kuwakumbuka katika huduma yao sawa na wao watakavyowakumbuka waumini hao katika maombi.

0 comments:

Post a Comment