Mjini Daslaam Tanzania watu wa type hii huwa tunawaita Mapedeshee, naongelea wale jamaa wenye pesa nyingi nyingi mpaka wanazigawa sana kwenye makumbi ya starehe na kwa watu wengine batani hope utakuwa umeshanisoma nini namaanisha, Hapa namuongelea Dallas ambae awali alikuwa na mahusiano na nyota wa Bongo Movie Jackline Wolper na baadae kuachana, Dallas alipata umaarufu sana kwa style yake ya kugawa pesa kwa wasanii pia kwa kutoka na star huyo Binti wa Wolper, aliishi maisha ya starehe tena ya kipedeshee sana kwa kutumia pesa mingi mingi na kununulia wasanii magari, lakini hali imekuwa tete sasa kwa Pedeshee huyo baada ya kuhisiwa kuwa zile pesa zimeisha kama sio kupungua hivyo kupelekea kuuza gari zake alizokuwa anamiliki, pia kipindi flani ilivuma sana kuhusu msanii Bob Junior kupokonywa gari alilonunuliwa na Dallas, yote hayo yaliongelewa lakini katika hali ya sintofahamu jana nilipokuwa uwanja wa taifa naangalia mechi nikamuona jamaa akiingia mmh! hakuwa ule niliemfahamu mwanzo ambae sura iling'aa kwa pesa kidogo kulionekana na hitilafu kwake hata muonekano wake hakuwa smart kivile. Ila yote ni mapito tu Dallas wa Wolper sasa ameshasahaulika.
0 comments:
Post a Comment