MSANII wa muziki wa kizazi kipya Hamis Mwinjuma 'Mwana Fa' aeleza, kuwa na kipaji zaidi ya kimoja ndiyo sababu ya kipekee inayomtofautisha yeye pamoja na kazi zake na baadhi ya wasanii wengine wa muziki wa bongofleva
Aliyazungumza
hayo jijini Dar es Salaam wakati akielezea mikakati yake aliyokuwa nayo
ya kuiachia nyimbo yake mpya hivi karibuni inayoitwa 'Kama Zamani'ambapo
mashabiki wake watapata fursa ya kuisikia nyimbo hiyo katika vituo
vya redio mbalimbali nchini, alisema kipaji ndicho kinachompa fursa ya
kufanya muziki katika ngazi ya kimataifa
Alisema muziki unamatawi mbalimbali kwani kuna baadhi ya wasanii wanakipaji cha kuimba tu lakini hawezi kufanya shoo katika 'stage' wapo baadhi wanajua kuandika na hawajui kuimba wapo wengine wanajua kufanya vyote kwa wakati mmoja
Akizungumzia kwa upande wake Mwana Fa alisema amejaaliwa kuwa na vipaji vyote kwa wakati mmoja huku akiwa na uwezo wa kuandika mashairi, kuimba pamoja na kulimiliki jukwaa pindi awapo katika shoo
"Nimejaliwa vipaji vyote hivyo, kwani nina uwezo wa kuandika mistari mizuri, kuimba na kulimiliki jukwaa na ndio maana shoo zangu zinakuwa na mvuto wa kipekee kutokana, sanaa na ubunifu niliokuwa nao "alisema Mwana Fa
Akizungumzia ujio wa wimbo wa 'Kama zamani' wenye mahadhi ya Hip Hop ambapo msanii huyo amewashirikisha baadhi ya wasanii kama Man'dojo, Domokaya na The Kilimanjaro Band (Wana Njenje), alisema kuwa ameamua kushirikisha wasanii hao ili kuleta radha tofauti ya muziki na mashabiki wapate muziki ulio bora

0 comments:
Post a Comment