Wema Sepetu na Kajala Masanja katika pozi mbalimbali.
Ile HURKA ya wanawake wengi kuwaambia mashoga zao siri zao nzito inadaiwa kumfanya msanii maarufu wa filamu Bongo, Wema Sepetu kufunguka kuwa, bila kuwa karibu na Kajala Masanja itakuwa ni kama kuamua kutembea mtupu.
Wema alifikia hatua ya kutoa maneno hayo katikati ya wiki hii kwa kuposti picha kwenye mtandao wa Instagram ikimuonesha yeye, meneja wake Martin Kadinda na Kajala huku akisindikiza na ujumbe mzito uliosomeka:
“I always call my poch and I fell so naked without, I need her everywhere with me. I hope that’s how they out each other.”

Aliandika kimombo, alimaanisha nini?
Tafsiri ya maneno hayo ni kwamba, Wema anamchukulia Kajala kama pochi yake na bila yeye anajihisi yuko uchi kiasi kwamba anataka kila sehemu wawe wote.
Kajala amjibu
Baada ya Wema kutundika ujumbe huo, Kajala naye alijitutumua na kutupia maneno ya kumshukuru (Wema) huku akieleza kuwa, kama ni hivyo yeye hana la kusema.
“Nimeyapenda maneno hayo, kama ni hivyo mimi sina la kusema,” aliandika Kajala kwenye mtandao huo.

0 comments:
Post a Comment