Wachunguzi wa Umoja wa Mataifa
wanajiandaa kurejea nchini Syria kuendelea na uchunguzi kuhusu ikiwa
silaha za kemikali zilitumika katika miji mingine ya nchi hiyo mbali na
Damascus.
Sasa wanajiandaa kutembelea maeneo mengine matatu ambako inaaminika silaha za sumu zilitumika ingawa kwa kiwango kidogo mapema mwaka huu. Shambulizi lilifanyika katika eneo la Aleppo,mjini Homs na karibu na Damascus.
Serikali ya Syria pamoja na waasi zinatuhumiana kwa kufanya mashambulizi .Wachunguzi hao wataamua ikiwa silaha za kemikali zilitumika lakini hawatasema ni nani wa kulaumiwa.
0 comments:
Post a Comment