Decoration & Catering Services

Decoration & Catering Services

Boutique

Boutique

Thursday, October 3, 2013

Gadiel Mpungu, kuja na albamu kali ya nyimbo za Injili.

Paul Clement

 Paul Clement, Gadiel Mpungu, Angel Bernad pamoja na rafiki mmoja, baada ya kurekodi.

 Gadiel katika pozi, akitathimini kazi waliyoirekodi.

Michael Manoni, sound engineer( wa kwanza kulia) akiwa na waimbaji waliyoshirikishwa katika albamu ya Gadiel.

Mwanamuziki mpya wa nyimbo za Injili hapa nchini, Gadiel Mpungu, leo ameiambia blog hii kuwa kwasasa anamalizia kutengeneza albamu yake ya kwanza ya nyimbo za injili, anayoamini kuja kufanya vyema sana hapa nchini.

Gadiel amesema kuwa mpaka sasa anataraji albamu yake kuwa na nyimbo nane, zilizo katika mahadhi kama ya mduara, rumba, zouk pamoja na ile style pendwa kutoka kusini mwa Afrika, ya kwaito.

Aidha mpaka sasa ndani ya albamu hiyo, Gadiel amemshirikisha mwanadada nguli wa muziki huu wa Injili, Angel Bernad ambaye pia ndiye mwalimu wake, pamoja na Paul Clement.

Ablamu hiyo inarekodiwa ndani ya studio za Jungle record zilizopo Sinza kwa Remmy, na kusimamiwa na Sound engineer Michael Manoni, huku muziki ukipigwa na Sam Mboya kwa upande wa kinanda pamoja na solo guita.

0 comments:

Post a Comment