Decoration & Catering Services

Decoration & Catering Services

Boutique

Boutique

Monday, November 4, 2013

Mzee wa Upako amtunishia misuli Tb Joshua.

 Mzee wa Upako

Tb Joshua

Baada ya Nabii wa Nigeria Tb Joshua kutabiri kuwa kuna nchi jirani na Kenya itakayopata pigo la kutekwa kwa Rais wake huku watu laki moja wakipoteza maisha kutokana na kuvamiwa na kundi la Al-Shabab, Mchungaji maarufu hapa nchini, Antony Lusekelo, ameinuka na kuupinga utabiri huo.

Hayo yalijiri jana katika ibada ya Jumapili, ambapo Mchungaji Antony Lusekelo alisema kuwa hiyo ni janja ya nabii huyu, ya kujitafutia wafuasi katika nchi mbalimbali kwa vitisho.

Aidha Mzee wa Upako amewataka Watanzania wote kuishi bila hofu wala mashaka, kwani ana imani sana na majeshi yote ya Tanzania, na kuwa hata kama kundi hilo litataka kufanya uvamizi huo, kamwe halitofanikiwa, kwa kuwa pia yupo yeye alilindaye Taifa hili katika ulimwengu wa roho.

Mzee wa Upako ni moja kati ya wahubiri wachache waliyopo duniani, wenye upako wa ajabu, aliyesimamisha Elinino mwaka jana hapa nchini.

0 comments:

Post a Comment