Polisi wakilinda doria mjini Paris,Ufaransa
Msako umeanzishwa mjini Paris, Ufaransa baada ya mtu
mmoja mwenye silaha kushambulia ofisi za gazeti la Liberation na
kufyatua risasi nje ya benki ya Societe Generale.
Mpiga picha huyo ambaye hakutajwa jina lake, anasemekana kuwa mpiga picha msaidizi wa kujitegemea ambaye alikuwa ndio tu anawasili katika ofisi za gazeti hilo tayari kwa kazi ya kupiga picha za mitindo.
Polisi wanamtafuta mtu ambaye aliingia kwa nguvu katika ofisi za kituo cha televisheni cha BFMTV Ijumaa.
Polisi kwa sasa wamepiga kambi nje ya ofisi zote za vyombo vya habari vikubwa mjini Paris.
Gazeti la Liberation limesema picha za mtuhumiwa wa tukio katika ofisi zao, zinafanana na picha za mtu aliyeshambulia kituo cha televisheni cha BFMTV.
Waziri wa mambo ya ndani wa Ufaransa, Manuel Valls, amekaririwa akisema "maadam mtu huyu bado hajakamatwa, na hatujui nia yake, hali hii inasababisha hali ya wasiwasi. Ni lazima tusonge mbele haraka katika kumkamata".
Bwana Valls amesema mtuhumiwa ana umri wa kati ya miaka 40 na 45 na amenyowa kipara.
Waziri Manuel Valls alitembelea eneo la tukio akifuatana na waziri wa Utamaduni Aurelie Filippetti na meya wa jiji la Paris Bertrand Delanoe.
Rais Francois Hollande amemtaka Bwana Valls kufanya kila liwezekanalo kumdhibiti mtu huyo ambaye anatuhumiwa kufanya mashambulio na kujua sababu za mashambulio hayo.
0 comments:
Post a Comment