Utata umezuka kufuatia kifo cha Suleiman Ally, 23, aliyekuwa mfungwa katika Gereza la Segerea kisha kuhamishiwa Gereza la Ukonga jijini Dar es Salaam na baadaye kufariki katika mazingira ambayo wazazi wake wanasema yamegubikwa na utata.
Habari zilizopatikana kutoka katika vyanzo vyetu zinasema kuwa marehemu alikuwa anatumikia kifungo cha miezi sita jela kutokana na makosa ya kukutwa na misokoto miwili ya bangi.
Aidha, habari hizo zinasema kuwa marehemu alikuhukumiwa kwenda gerezani Septemba 8 mwaka huu na Mahakama ya Mwanzo ya Kawe jijini Dar.
Aidha, habari hizo zinasema kuwa marehemu alikuhukumiwa kwenda gerezani Septemba 8 mwaka huu na Mahakama ya Mwanzo ya Kawe jijini Dar.
Mama mzazi wa Suleiman aliyejitambulisha kwa jina la Habiba Seleman Kipaza aliliambia gazeti hili kuwa taarifa za kufariki dunia kwa kijana wao walizipata Desemba 25 saa 12 jioni lakini jitihada zao zilisema alifariki Desemba 17 mwaka huu.
“Sisi kuchelewa kupewa taarifa ya kifo kumezua maswali mengi kutokana na kuwa hakukuwa na sababu ya kukaa siku zote hizo bila wazazi au ndugu kujulishwa,” alilalamika mama huyo.
Kwa upande wake, baba mzazi wa marehemu aliyejitambulisha kwa jina la Suleiman Ally Masungu alisema kuwa mwanaye hadi anaenda kutumikia kifungo hicho alikuwa mzima na hajawahi kulalamika kuumwa ugonjwa wowote hata walipokuwa wakimtembelea.
“Mimi kilichonisikitisha ni ndani ya jeshi la magereza ni kukosa kutueleza ukweli juu ya kifo cha mwanangu.
“Baada ya kupata taarifa ya kifo kuwa amefariki Desemba 25 mwaka huu tulikwenda Hospitali ya Muhimbili lakini tukaambiwa aliletwa pale Desemba 17 akiwa maiti.
“Baada ya kupata taarifa ya kifo kuwa amefariki Desemba 25 mwaka huu tulikwenda Hospitali ya Muhimbili lakini tukaambiwa aliletwa pale Desemba 17 akiwa maiti.
“Hata siku ya kuchukua maiti kwa ajili ya maziko tulimkuta akiwa ametokwa na damu puani pamoja na majeraha sehemu za shingoni kitu ambacho kimenitia shaka juu ya kifo chake.
“Marehemu alivuliwa nguo za magereza siku tuliyoenda kuchukua mwili wake mochwari hali ambayo pia inaashiria kuwa Suleimani alikuwa amefikishwa pale akiwa amekufa.
“Marehemu alivuliwa nguo za magereza siku tuliyoenda kuchukua mwili wake mochwari hali ambayo pia inaashiria kuwa Suleimani alikuwa amefikishwa pale akiwa amekufa.
“Niliambiwa na askari magereza kuwa mwanagu alikuwa amelazwa hapo hospitali kabla ya kifo nikawa najiuliza kama alikuwa amelazwa kwa nini nimemkuta mochwari akiwa na nguo za magereza?,” alihoji mzee Suleimani
Ameziomba taasisi za haki za binadamu na vyombo vya dola kufuatilia suala hilo akiamini kuwa kuna kitu magereza wanaficha ukweli licha ya wao kufuatilia Gereza la Ukonga.
Gazeti hili lilimtafuta Msemaji wa Jeshi la Magereza nchini, Omari Mtanga ambaye hakupatikana na taarifa zilisema amehamishwa.
Gazeti hili lilimtafuta Msemaji wa Jeshi la Magereza nchini, Omari Mtanga ambaye hakupatikana na taarifa zilisema amehamishwa.
Hata hivyo afisa mmoja wa jeshi hilo ambaye hakutaka jina lake liandikwe gazetini kwa kuwa siyo msemaji alisema marehemu alihamishiwa Ukonga kwa uhamisho wa kawaida akitokea Gereza la Segerea.
“Marehemu aliugua na akapelekwa Hospitali ya Muhimbili kwa matibabu zaidi baada ya kutibiwa ndani ya magereza kwa wiki nzima,” alisema afisa huyo.
Afisa huyo aliongeza kuwa mfungwa yeyote anapofariki kuna utaratibu za kidaktari zinafanywa kabla ya kupelekwa mochwari na kama familia inasema ina shaka basi hata mochwari wasingempokea.
“Familia ya wafiwa isiwe na shaka, kama ni suala la kuchelewa kupata taarifa basi kulitokana na jitihada za kupata hao wazazi wanakaa wapi maana marehemu alikuwa hakai na wazazi wake,” alisema.
Marehemu alizikwa Desemba 27 mwaka huu katika Makaburi ya Chanika Mahelahela njia panda ya Tegeta jijini Dar.
Chanzo: Uwazi.
0 comments:
Post a Comment