Decoration & Catering Services

Decoration & Catering Services

Boutique

Boutique

Friday, January 3, 2014

MICHEZO: PSPF kudhamini Tanzania Boxing Awards.

 Uongozi wa PSPF Tanzania Boxing Awards wakiwa pamoja na Meneja wa uchangiaji wa hiari PSS.

Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi PSPF Boxing Awards, Said Masanga akiongea na waandishi (katikati), Mwajaa Iddi Sembe, Meneja mipango wa uchangiaji wa hiari PSS (kulia) na Mutta Rwakatare, Mwenyekiti msaidizi wa kamati ya maandalizi PSPF Tanzania Boxing Awards. 

 Mwajaa Iddi Sembe, Meneja mipango wa uchangiaji wa hiari PSS



 Waandishi wa habari.


Mfuko wa pensheni wa PSPF kupitia mpango wake wa uchangiaji wa mafao kwa hiari yaani PSS, leo wametangaza kudhamini michuano ya ndondi nchini yaani Tanzania Boxing Awards.

Akielezea michuano hiyo Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi, Said Masanga amesema kuwa hizi zitakuwa ni ngumi za wazi tofauti na zile zinazochezwa ndani ya ukumbi na kuwa na kiingilio kama ilivyozoeleka, huku lengo lao likiwa ni kutoa burudani kwa wananchi wote na kuwapa nafasi mabondia wachanga kushiriki katika kinyang`anyiro hicho.

Na kwa upande wa PSPF kupitia mpango wa uchangiaji mafao kwa hiari PSS, Meneja wa mpango huo Bi Mwanjaa, amesema kuwa wameamua kudhamini michuano hiyo kwani hata mabondia nao wanaweza kushiriki katia mfuko huo wa mafao, hususani kwenye huo mpango wa kuchangia kwa hiari wa PSS.

Aidha katika kuelezea jinsi washindi wa michuano hiyo watakavyopatikana, kamati hiyo imesema kuwa wananchi watawachagua mabondia wao wanaowapenda kwa kutuma ujumbe mfupi kwenda namba 15573,ujumbe utakaompa ushindi bondia kwa asilimia 40, huku asilimia 60 zikitoka kwa makocha na waamuzi wa mashindano hayo.

Mchezo wa bondia ni moja kati ya michezo iliyoiletea Taifa letu heshima kama ile iliyoipata kwa bondia mashuhuri na mahiri hapa nchini, Fransis Cheka aliyeshinda ubingwa wa dunia wa WBF mwaka jana.

0 comments:

Post a Comment