Decoration & Catering Services

Decoration & Catering Services

Boutique

Boutique

Monday, February 24, 2014

Duh! Kumbe Linex ni shabiki mkubwa sana wa Ambwene Mwasongwe?


Linex

Ambwene Mwasongwe

Kwa taarifa yako, kama ulikuwa hufahamu ushabiki uliyojificha kwa kijana huyu maarufu kutoka Kigoma yaani Linex, ni kwamba yeye ni shabiki mkubwa mno wa mwanamuziki wa nyimbo za Injili kutoka Mbeya, anayetamba kwa a.k.a ya Mzee wa majaribu ni mtaji, Ambwene Mwasongwe.

Mmoja kati ya waandishi wetu alilibaini hilo hivi karibuni, ambapo yeye alikuwa akiitembelea mara kwa mara Studio maarufu hapa nchini inayotambulika kwa jina la Empty Soulz, mahali ambapo ni maskani makubwa ya Linex, ambapo karibia kila siku alizo bahatika kukutana na Linex, alikuwa akimsikia akiziimba nyimbo za Ambwene Mwasongwe, hususani zile zilizopo kwenye toleo lake jipya.

'Siyo siri kaka, asikuambie mtu, huyu jamaa namkubali kweli hususani kwenye hii albamu yake ya sasa, ila kwa upande mwingine namuonea huruma kuwa sijui kama ataweza kutengeneza kitu kikali namna hii' alisikika akisema Linex.

Hata hivyo hatuna uhakika kama Ambwene analitambua hili au kuwa naye anazipenda kzi za Linex 

0 comments:

Post a Comment