Pichani: Harris Kapiga muanzilishi wa Gospel Club.
Ni katika hali ya kushtusha sana tena kuogofya kwa wafuasi wa dini ya Kikristo yaani Wakristo, ambapo mmoja kati ya wanahabari waliyowahi kutangaza katika redio ya dini ya Kikristo hapa nchini (Praise Power Radio), na kupata umaarufu mkubwa kutokana na uwezo wake wa kuweza kuchambua na kulidadavua vyema neno kutoka ndani ya Biblia takatifu, kufungua Club ya Kikristo aliyoipa jina la Gospel Club.
Nje kabisa na maandiko ya dini hii, Harris Kapiga ambae kwasasa ni mtangazaji wa Clouds Media Group na mchungaji wa kanisa lake lililopo maeneo ya Sinza, amefungua Club hiyo ambapo mashabiki wa kituko hicho cha kiroho, huruka majoka tangu jioni mpaka majogoo.
Club hiyo iliyopo mitaa ya Mbezi, ilifunguliwa rasmi mwishoni mwa mwaka jana na kuwa gumzo kwa kila Mkristo alyezipata habari hizo, jambo lililotutia hamasa ya kutaka kuijua Club hii ya kilokole ikoje.
Mazingira yake yakoje?
Upatapo bahati ya kufika na kuingia ndani ya Club hii, utakutana na giza kubwa lililonakshiwa na taa za kumbi za starehe (Disco light), huku ukipokelewa na sofa mbili za kujipumzisha zilizotenganishwa na meza fupi katikati, viti virefu, na ukunjapo kushoto utakutana na danse floor ambapo kwa mbele ya mlango wa kuingilia hapo, kuna Counter ya vinywaji na mkono wa kushoto wa mlango wa kuingilia sehemu hiyo ya kujimwaya mwaya, utakutakutana na DJ, anayecharaza nyimbo za dini.
Lakini utokapo nje ya Club hii, mkono wa kushoto yupo babu anayechoma mishikaki na kwenye jengo hilo hilo ipo Bar kubwa inayopiga nyimbo za duniani kama Number one ya Diamond, Closer ya Vanessa Mdee N.K na kuuza vilevi vya kila namna.
Watu wakiyarudi
Viti vya kupumzika
Muonekano halisi
Kila Mkristo aliyefika katika ukumbi huo wa starehe za kiroho, au aliyezisikia habari za ukumbi huo humshangaa sana Harris kwa kuanzisha na kukipigia debe kitu ambacho wamekiita ni Upuuzi na uchanga wa kiroho aliyo nao Mchungaji huyu.
Wengine wamekitafsiri kitendo hicho kama mawazo mapotofu na takataka za duniani zilizosalia ndani ya Mchungaji huyu wa kanisa lake changa lililopo Sinza, kwani yapo mawazo mengi mazuri ya kutengeneza vitu vilivyo na heshima ndani ya dini hii.
"Yani siyo siri hapa Harris kachemka vibaya mno, tena hii inadhihirisha uchanga aliyo nao kiroho mtu huyu ajiitaye Mchungaji. Mimi nilipoingia tu humu ndani nilihisi nipo kuzimu. Kwa kweli siwezi kuimba wala kuendelea kukaa humu sawa na alivyo nialika mimi na timu yangu ya wanamuziki" hayo yalisemwa na mwimbaji maarufu wa muziki wa Injili hapa nchini, aliyeomba jina lake lisitajwe.
"Yani kaka ningejua kama huduma yenyewe ndiyo hii, nisingekuja. Guys! mimi ninapigaga giggs zakutosha katika club za burudani, kwenye bendi za watu maarufu wa duniani, lakini hii imetia fora, yaani ni zaidi ya club za duniani. Na hata Wazungu na udigitali wao wote waliyo nao hawajawahi kuwa na kitu kama hiki, sasa sijui amekitoa wapi yeye, au sijui hajaridhishwa na mikesha ya makanisani au uwanja wa taifa tuifanyayo? sijui yani ila nimemshangaa mno" alisema moja kati ya wanamuziki waliyoshindwa kuhudumu siku hiyo ambayo muandishi wetu alifika ukumbini hapo.
Vijana wakiyarudi ilikuwa ni saa tatu usiku hapa
Je, lipo andiko linaloruhusu kitu kama hicho?
"Katika kusoma kwangu kote Biblia sijawahi kutana na andiko linalo ruhusu kitu hiki. Hapa Harris anawapotosha wakristo waziwazi, na tena anadhihirisha kuwa hizi ni siku za mwisho zilizonenwa" alisema mfuasi wa dini hii ya Kikristo aliyetambulika kwa jina moja la John.
Hata hivyo muandishi wetu alishindwa kuzungumzana Harris kutokana na Mchungaji huyo kuwa bize sana na baadhi ya watu waliyoketi nae usiku huo nje ya Club hiyo, huku mwingine akisikika kumwita Pastor ambae kwa pamoja walikuwa wakipiga gumzo (yani yeye, na Pastor mwenzie na wadau wao), huku wakila mishikaki na kuywa soda.
0 comments:
Post a Comment