Decoration & Catering Services

Decoration & Catering Services

Boutique

Boutique

Sunday, February 23, 2014

Kundi la Soul Music Gospel (SMG) lafanya tamasha leo.

 Tulianza na nyimbo za kusalimiana.

 Oggy Keyz akisalimiana na mmoja wa wadau wa muziki wa injili.

 Moja kati ya makundi yaliyo tumbuiza. 

 Oggy, Emma Bezy, Melisa na mmoja kati ya wadau wakubwa wa kundi la Glorius Worship Team.

 Bomby Johnson pamoja na Paul Clemet dakika chache kabla ya wao kupanda jukwaani.

 Victor wa SMG akicharaza kinanda.


Mwanadada huyu naye, aliguswa sana na nyimbo zilizokuwa zikiongozwa na kundi la SMG.

Alex Kisonga wa GWT, akimtafakari Mungu kwa kupitia ujumbe aliyokuwa akiusikiliza kwa njia ya uimbaji.

 Kaka huyu nae alikutwa na kamera yetu akibubujika.

 Alex Kisonga na Emmanuel  Mabisa wa GWT wakiyarudi.

Emma Basse, Bomby Johnson, pamoja na Emma Gripa wakihudumu.  

 Emma Gripa akifanya yake kwa furaha tele.

 Baraka Ngowi naye hakusita kuonyesha alicho nacho.

Oggy Keyz tayari kuwajibika. 

Paul Clement naye alihudumu.

 Emma Basse aking'ata menoooo! Baghaaaaa


 Soul Music Gospel wakihudumu sasa.

 Wapigaji wa SMG wakitikisa jukwaa.


Kundi la muziki wa Injili lenye idadi ya watu 20 na umri wa miezi 9, Soul Music Gospel, leo limefanya tamasha katika Kanisa la EGM, Kinondoni huku lengo lao haswa likiwa ni kuwaunganisha watu wote ili kumsifu na kumuabudu Mungu, kama lilivyo lengo la kundi hili.

Aidha kundi hili ambalo mpaka sasa limekwisha fanikiwa kuwafikia watu mbalimbali wa Mkoani Dodoma (Kondoa), Kibaha (Maili moja) na kwingineko, linasumbuliwa na changamoto za ukosefu wa mahali pa kufanyia mazoezi pamoja na vifaa vya muziki kwaajili ya kazi yao hiyo, kwani mpaka sasa hutegemea vitu hivyo kutoka kwa watu mbalimbali wanao wasaidia, hususani kanisa la Living Water Kibaha kwa Mchungaji Pascal.

Kundi hili ambalo limewaburudisha sana watu waliyofika Kanisani hapo EGM, lilianzishwa na vijana wanne ambao ni Victor Daniel, Moses Edrad, Grayson Bruno, Joseph Kitambo waliyokutana
 wakiwa Casfeta, mwaka 2009.

0 comments:

Post a Comment