Decoration & Catering Services

Decoration & Catering Services

Boutique

Boutique

Monday, April 28, 2014

'Victor Daniel' aanza kuwa tishio kwenye 'Gospel'


Hatimae ndoto ya mpiga kinanda mahiri Victor Daniel yaanza kutimia, baada ya mkono wake kuanza kupendwa na kushirikishwa katika kazi mbalimbali.

Victor mwenye umri kati ya miaka 20-25 (umri umeifadhiwa), kwa mwaka huu amefanya kazi nyingi sana katika muziki wa Injili kwa hapa Tanzania, zikiwemo zile nyimbo za mwanamuziki Gadiel Mpungu alizo charaza vyema kinanda, kiasi cha kuwa gumzo katika tasnia. Kazi nyingine alizo zifanya ni pamoja na kwenye tamasha la pasaka la mwaka huu ambapo yeye alishiriki katika upigaji wa muziki wakati wa perfomance ya Jesca BM, Upendo Nkone, Sara K, na Glorius celebration.

Kwa wasiyo mfahamu kijana huyu, basi tabia yake ni mcheshi kiasi, mstaarabu, mvumilivu na mwenye utu, mwenye kuithamini na kuipenda sana kazi yake na huduma Mungu aliyo iweka ndani yake zaidi ya fedha.

Kwa mawasiliano nae ya kikazi, mpigie simu namba;+255 655 267 872 au mfuate Facebook kwa jina hilo la Victor Daniel.

0 comments:

Post a Comment