Decoration & Catering Services

Decoration & Catering Services

Boutique

Boutique

Sunday, August 10, 2014

Mumewe Mbasha atelekeza hata marafiki wa karibu.


Mume halali wa mwanamuziki wa muziki wa Injili hapa nchini Flora Mbasha, ndugu Emmanuel Mbasha, kwasasa inaelezwa kuwa amejitenga kabisa na marafikize waliyokuwa karibu kipindi cha mwanzo.

Hayo yameelezwa leo na mmoja kati ya waliyowahi kuwa washambulia jukwaa wake, huku akionyesha hali ya kusikitishwa sana na kitendo hicho pamoja na kumuonea huruma.

"yaani kaka ninavyo ongea na wewe, nina kama mwaka sasa sijaonana na bro Emmanuel Mbasha, na tangu litokee hili sakata lake la juzi, ndo kabisa hata nikimpigia simu au kumtumia msg japo nimtie moyo kama mdogo wake aliye nikuza katika tasnia, hata hapokei" alisema kijana huyo (jina limehifadhiwa).

Aidha kijana huyo pia aliongeza kuwa katika sakata hili la Mbasha na Mkewe, "jazba" zao zinaweza zikawa ni chanzo kikubwa cha wao kufika hapo walipofika, kwani kuna wakati walikuwa wakigombana kwa vitu vidogo sana kitu ambacho kama mmoja kati ya wawili hao hakuwa na akili iliyo tulia, basi angeweza fanya maamuzi ya ajabu kama haya ya sasa, yaliyo idhalilisha tasnia ya muziki wa Injili hapa nchini.

Emmanuel Mbasha na mkewe Flora, walingia kwenye mgogoro mkubwa wa ndoa, ambapo Emmanuel alishukiwa kumbaka mdogo wa mwanadada huyu aliyewahi tamba na kibao chake cha " Jipe moyo", huku Emmanuel akikanusha madai hayo kwa kusema kuwa ni njama zilizo tengenezwa ili kuwatenganisha kwani kwasasa mkewe ana mahusiano na kiongozi mmoja wa kiroho hapa nchini.

0 comments:

Post a Comment