Decoration & Catering Services

Decoration & Catering Services

Boutique

Boutique

Monday, August 4, 2014

"Mzee wa Upako" Antony Lusekelo akiri wazi kuwa yeye si nabii.

Mchungaji mkuu wa kanisa la GRC Ubungo Kibangu, Antony Lusekelo alimaarufu kama Mzee wa Upako, akiri hadharani kuwa yeye si Nabii bali ni Baba Mchungaji.

Mzee wa Upako aliyasema hayo jana katika ibada ya Jumapili alipokuwa akieleza jinsi anavyo kerwa na tabia za baadhi ya watumishi kujipa majina makubwa kuliko kazi wanazo zifanya.

Aidha Mzee wa Upako alisisitiza kuwa, kama mtumishi wa Mungu hupaswi kujitetea na kujikinga kwenye majina makubwa na badala yake kufanya kazi ya Mungu kwa uaminifu na kisha matunda ya kazi yako ndo yaeleze wazi kuwa wewe ni nani.

Kwasasa mtumishi huyu wa Mungu mwenye umahiri wa kuhubiri ipasavyo, ndiye mwenye kibali kikubwa hapa nchini tangu kwa watoto, vijana, watu wazima na hata viongozi wa nchi.

0 comments:

Post a Comment