Dk. Shukuru Kawambwa.
Nyumba zaidi 120 zimevunjwa katika zoezi la bomoabomoa lililofanywa na Wakala wa Barabara Tanzania (Tanroads) Mkoa wa Mbeya ili kupisha ujenzi wa Barabara ya Mbeya– Chunya na kusababisha wakazi zaidi ya 400 katika kata za Iganzo na Isanga kukosa makazi.
Zoezi hilo lilifanyika jana kuanzia saa 1:30 asubuhi chini ya ulinzi mkali wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU).
Baadhi ya waathirika walilalamikia zoezi hilo kwa madai kuwa baadhi yao hawajalipwa fidia licha ya serikali kukamilisha tathmini ya nyumba na mali zao.
Mwenyekiti wa waathirika hao, Timoth Mwambapa, alisema fidia haikutolewa kwa haki kutokana na baadhi yao kulipwa fedha nyingi na wengine kutolipwa kabisa.
Alisema malalamiko yao waliyafikisha kwa aliyekuwa Waziri wa Miundombinu, Dk. Shukuru Kawambwa, ambaye aliwatembelea na kuagiza zoezi la kufanya tathmini ya nyumba na mali zao ili zoezi lilrudiwe.
Hata hivyo, alisema agizo hilo halikutekelezwa na watendaji wa Tanroads Mkoa wa Mbeya.
Makamu Mwenyekiti wa waathirika hao, Ismail Mwaipaja, alisema suala hilo tayari wamelifikisha katika Mahakama Kuu Kanda ya Mbeya na Mahakama ilitoa hati ya kuzuia ubomoaji wa nyumba zao, lakini Serikali imekiuka amri hiyo.
Msimamizi wa zoezi, ofisa wa Tanroad Mkoa wa Mbeya, aliyejulikana kwa jina moja la Mkina, alikataa kuzungumzia suala hilo kwa madai kuwa yeye sio msemaji wa Tanroads.

0 comments:
Post a Comment