Nakuru. Katika hali isiyo ya kawaida wanandugu watano kutoka familia moja wamefunga ndoa siku moja nchini Kenya.
Tukio hilo lililoibua mshangao miongoni mwa watu walioshuhudia lilitokea katika kanisa la mtakatifu Peter mjini Nakuru.
Maharusi waliojawa na furaha isiyo na kifani walielezea kuwa malezi yao bora yaliwafanya wote kuchagua kufunga ndoa siku moja.
Samson Wachira, ambaye ni wa kwanza kuzaliwa
alisema wazazi wao waliwaonyesha kupendana na kushirikiana katika mambo
yote tangu wakiwa wadogo hali iliyowapelekea kukua katika mazingira
hayo.
Hivyo basi, Wachira alielezea kuwa kila mmoja wao alipotaka kufunga ndoa rasmi, aliwaita nduguze kwa ushauri.
Wachira ana mika 36 ilhali George Wango, ambaye ni wa mwisho kuzaliwa ana umri wa miaka 24.
Wengine walikuwa Peter Mbugua, 35, Stephen Kinyanjui, 34, na Harman Kago,32.
Ndugu hao waliitaja siku hiyo kama ya furaha
ambayo walikuwa wakiingojea kwa hamu kubwa kutokana na kufikia kupiga
hatua moja maishani mwao .
“Tumekuwa tukiingoja na kujitayarisha kwa siku hii kwa mwezi mmoja uliopita,” alisema Wango, mmoja wa maharusi hao
Wazo la kufunga ndoa siku moja liliwajia ndugu hao
miezi saba iliyopita wakati kasisi mmoja alipowatembelea nyumbani kwao
eneo la Kiratina.
Baba yao aliandaa karamu na ibada ya misa ya
shukrani wakati kasisi alitaka kujua ni nani kwa familia hiyo alikuwa
amekubaliwa kupokea sakramenti.
Kulingana na desturi za kanisa la Katoliki, ni
sharti mwanamume awe amefunga ndoa rasmi kanisani ili kuruhusiwa kupokea
sakramenti hivyo kasisi huyo aliwapa changamoto vijana hao kuhusu faida
za kufunga ndoa kanisani.
0 comments:
Post a Comment