MAHAKAMA ya Wilaya ya Ludewa, mkoani
Njombe, imemhukumu kifungo cha miaka 30 gerezani na kuchapwa viboko 30 mwalimu
wa Shuile ya Msingi Ingwachanya.
Mwalimu
huyo, Bw. Romanus Msango, mkazi wa Lupembe, wilayani Njombe, alitiwa hatiani
kwa kosa la kumbaka mwanafunzi wa miaka 14 (jina linahifadhiwa) na kumuumiza
vibaya sehemu za siri.
Akisoma
hukumu hiyo Septemba 6 mwaka huu, Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya
ya Ludewa, Bw.
Fredrick
Lukuna, alisema mahakama imeridhika na ushahidi uliotolewa na upande wa
mashtaka ambao haukuwa na shaka yoyote.
Alisema
mshtakiwa alitenda kosa hilo
kinyume na kifungu namba 1309(1) na 31(1) cha kanuni ya adhabu ya mwaka 2002
hivyo adhabu hiyo ni fundisho kwa wengine.
"Natoa
adhabu hii ili kukomesha vitendo hivi kwenye jamii
kwani
vinaleta madhara makubwa kwa watoto na wanawake pamoja na kusababisha magonjwa
ya kuambukiza," alisema.
Awali ilidaiwa na Mwendesha Mashtaka, Edison Kasekwa kuwa,
mshtakiwa alitenda ukatili huo wa kinyama Agosti 20,2012 katika Kijiji cha
Masimbwe, Kata ya Mlangali.
Alisema kabla
mshtakiwa hajatenda kosa hilo,
alimshambulia mwanafunzi huyo, kumbaka na kumlawiti jambo ambalo lilimsababishia
maumivu makali.
"Serikali ilimpa mshtakiwa dhamana
kubwa ya kulea watoto ambao ni nguvukazi ya Taifa la kesho lakini amewageuka na
kutenda kitendo ambacho ni kinyume na maadili ya kazi yake, kuidharirisha
taaluma hivyo naomba mahakama itoe adhabu kali iwe fundisho kwa walimu
wengine," alisema.
Bw. Kasekwa aliongeza kuwa, mshtakiwa
alikusudia kutenda makosa hayo kwa sababu alimfuata mwanafunzi huyo shambani
wakati akivuna mahindi na wenzake ambao walikimbia kwenda kijijini kutoa
taarifa baada ya mshtakiwa kumkamata mwenzao na kumpeleka kichakani.
Wa k a t i h u o h u o , wa
t u wawili Bahati Mtega na Flowin Mtweve, wote wakazi wa Milo,
wamehukumiwa kifungo cha maisha gerezani na kuchapwa viboko 12 kila mmoja kwa
kosa la kumbaka mke wa mtu na kumsababishia maumivu makali
0 comments:
Post a Comment