Decoration & Catering Services

Decoration & Catering Services

Boutique

Boutique

Thursday, October 10, 2013

Misri yatoswa misaada na Marekani


Marekani inataka Misri kuhakikisha uchaguzi huru na haki unafanyika kabla ya kuipa msaada tena

Serikali ya Misri imekosoa Marekani kufuatia uamuzi wake wa kusitisha awamu nyingine ya msaad wa kijeshi kwa serikali yake inayoungwa na jeshi la nchi hiyo.

Msemaji wa wizara ya mambo ya nje wa Misri amesema, taifa hilo haliwezi kuhujumiwa na uamzui huo akisema kuwa serikali ya Misri itaendelea na kile alichokitaja kama mkondo wake wa kuafikia utawala wa demokrasia.
Marekani ilibana sehemu kubwa ya dola bilioni 1.3 ambazo hutolewa kwa Misri kama msaada wa kijeshi.

Kutolewa kwa zana za kijeshi pamoja na msaada wa kifedha kwa serikali ya Misri itabanwa. Hii ni kwa mujibu wa taarifa ya mambo ya nje ya Marekani.
Imesema kuwa hatua lazima zichukuliwe katika kuhakikisha kuna uchaguzi huru na wa haki kama kikwazo cha kupata msaada huo tena.

Hataua hii inatokana na Marekani kudurusu hali nchini Misri baada ya maafisa wa utawala kumwondoa mamlakani Morsi na kusababisha idadi kubwa ya vifo miongoni mwa wafuasi wake.

"Tutatendelea kuzuia msaada mkubwa wa kijeshi kwa Misri hadi itakapochukua hatua za kuhakikisha kuna serikali halali mamlakani na ambayo imechaguliwa kihalali na kwa njia ya kidemokrasia,’’ alisema msemaji wa idara ya mamambo ya ndani wa Marekani Jen Psaki.

Maafisa walisema kuwa kubanwa kwa msaada huo, kutakosesha Misri kupata mamilioni ya dola pamoja na ndege aina ya Apache helikopta, pamoja na makombora ya Harpoon na sehemu za vifaru vya kijeshi.

Serikali pia inapanga kubana dola milioni 260 kwa serikali ya Misri pamoja na mkopo wa dola milioni 300.

Hata hivyo wadadisi wanasema kuwa hatua hii sio kali sana kwa Misri na kuwa ilitarajiwa hasa kutoipa Misri zana za kijeshi, na mafunzo ambayo pia hayatatolewa hadi masharti yatimizwe.

Aidha itaendelea kutoa msaada wa kiafya na elimu pamoja na kuakikisha kuwa usalama unadhibitiwa katika rasi ya Sinai.

0 comments:

Post a Comment