Decoration & Catering Services

Decoration & Catering Services

Boutique

Boutique

Thursday, October 10, 2013

Waziri mkuu wa Libya Zeidan atekwa nyara.


Waziri mkuu wa Libya ametekwa nyara na watu wasiojulikana na ambao walikuwa wamejihami kutoka nyumbani kwake mjini Tripoli.

Duru zinasema kuwa bwana Ali Zeidan ametekwa nyara na kupelekwa katika eneo lisilojukana , lakini hakuna taarifa zaidi kuhusu tukio hilo.

Baadhi ya ripoti zinasema kuwa huenda Zeidan amezuiliwa.
Kundi lililokuwa la waasi na ambalo lina uhusiano na serikali limekiri kumteka nyara Zaidan kufuatia kibali cha kumkamata kilichotolewa na kiongozi wa mashtaka .

Picha ya Zeidan akitekwa nyara mjini Tripoli

Lakini serikali ya Libya imekanusha madai hayo. Kituo cha televisheni cha Al Arabiya kimeonyesha picha za bwana Zaidan akitekwa nyara.

Habari zinasema kuwa Zeidan alitekwa nyara akiwa ndani ya hoteli ya kifahari anamoishi.

Serikali imekuwa ikikabiliwa na shinikizo kali baada ya makomando wa Marekani kumkamata mmoja wa viongozi wa al-Qaeda Anas al-Liby nchini Libya.

Bwana Zeidan alikamatwa Jumamosi mjini Tripoli kwa madai ya kuhusika na mashambulizi ya kigaidi yaliyofanywa dhidi ya balozi za Marekani nchini Tanzania na Kenya mwaka 2008.

Mnamo siku ya Jumatatu Libya ilimhoji balozi wa Marekani kuhusu kukamatwa Al Liby.

Kwa upande wake Zeidan alitoa wito kwa Marekani na nchi za Magharibi kuisaidia serikali ya Libya kukomesha vitendo vya wapiganaji wenye itikadi kali nchini humo.

Waziri mkuu huyo alisema kuwa nchi yake inatumia kama kivukio cha kusafirishia silaha kwenda katika maeneo mengine ya kanda hiyo.

0 comments:

Post a Comment