Decoration & Catering Services

Decoration & Catering Services

Boutique

Boutique

Wednesday, November 20, 2013

Karashani na Ndimara kuwafundisha waandishi wa habari wa Clouds.

Karashani
 
 Ndimara

Katika harakati za kuwaboresha waandishi wake, Clouds Entertainment wamiliki wa vyombo vya habari kama Clouds televisheni na Clouds Fm, wamewapa fursa waandishi wake wa habari, ya kuelimika kwa kuwatafutia waalimu wawili wa tasnia ya habari wanaowafundisha juu ya kuripoti katika mazingira tete au waweza sema mazingira hatarishi.

Walimu hawa ni Fili Karashani pamoja na Ndimara, ambao ni waandishi wabobevu, waliyowahi kufanya kazi zao katika mazingira tofauti tofauti yakiwemo hayo hatarishi, ndani na nje ya nchi.

Elimu hiyo inatolewa kwa mfumo wa warsha, iliyoanza tarehe 18 mwezi Novemba na kuhitimika kesho tarehe 21 Novemba.

0 comments:

Post a Comment