Decoration & Catering Services

Decoration & Catering Services

Boutique

Boutique

Sunday, November 24, 2013

Kijiji kimoja Kenya chatekwa.


Wanawake wa kabila la waturkana huko nchini Kenya

Serikali ya Kenya imeripotiwa kutuma maafisa wa polisi kuongeza ulinzi katika kijiji cha Lorokon kaskaskani mwa count ya Turkana mahali ambapo watu wenye silaha walikuwa wamezingira vituo vitatu vya polisi ambao pia inasemekana wamewataka wanavijiji.
Gavana wa eneo hilo Josephat Nanok amelimbia shirika la habari la Kenya KNA kuwa zaidi ya wanavijiji 900 wengi wao wakiwa ni wanawake na watoto walizingirwa na watu hao wenye silaha na kushindwa kutoka kwenda kutafuta chakula na maji.
Habari kutoka eneo la tukio zinasema ugomvi wa mpaka baina ya jamii mbili za makabila ya waturkana na wapotok ndio chanzo cha tukio hilo.
Awali iliripotiwa kuwa watu wenye silaha kutoka jamii ya kabila la wapotok wamezingira kijiji cha Lorogon kwa siku nne.
Televisheni ya Kenya iliripoti mazungumzo ya kutatua mgogoro huo kati ya makabila hayo yanayogombana yalitarajiwa kufanyika siku ya jumapili.

0 comments:

Post a Comment