Decoration & Catering Services

Decoration & Catering Services

Boutique

Boutique

Tuesday, November 5, 2013

Ras Inno kuiinua Raggae Tz.


Ras Inno akiwa ameshikilia moja kati ya tunzo zake za Kill Music Awards.

Baada ya kuimba muziki wa Raggae kwa miaka mingi hapa nchini, Innocent Nganyagwa alimaarufu kama Ras Inno, ameinuka na kuueleza mpango wake wa kutaka kuuinua muziki wa Raggae na kuufanya kuwa moja kati ya makimbilio machache ya wanamuziki wa hapa nchini.

Ras Inno aliyasema haya huku akionyesha hali ya kujiamini na kuwa na matumaini katika mpango wake huo, huku akiongeza kuwa kwa kulitimiza hilo basi ameamua kufungua kampuni inayoenda kwa jina la Raggae Production House, itakayojihusisha moja kwa moja na muziki huo, sanjari na kuzitetea haki zote za msingi anazotakiwa kuzipata mwanamuziki wa Raggae, wa hapa nchini.

Innocent Nganyagwa ni mmoja kati ya wasanii wachache waliyodumu katika aina hii ya muziki kwa hapa nchini, na kushinda tuzo mbalimbali, japo kuwa muziki huu wa Raggae haujapewa kipaumbele sana ukilinganisha na aina nyingine za muziki kama Bongo Fleva, Dansi, Taarabu pamoja na Hip Hop.
Kupitia blog hii basi tutakujuza mengi juu ya ujuo huo wa Ras Inno, pamoja na kampuni yake hiyo.

0 comments:

Post a Comment