Sifa na rambirambi zinaendelea kumiminika kwa familia
ya mwanamuziki,muimbaji na mtungaji mashuhuri wa muziki wa rumba Tabu
Ley Rochereau aliyefariki dunia Jumaamosi akiwa na umri wa miaka 76
katika hospitali moja nchini Ubelgiji.
Tungo zake zilivigusa vizazi kadhaa katika pembe zote za bara la Afrika na kwingineko duniani.Tabu Ley, ambaye pia alikuwa mwanasiasa hakupata nafuu tangu apate kiharusi mnamo mwaka 2008 na alizidiwa mwishoni mwa wiki kwa mujibu wa mwanaye Jean-Claude Muissa.
Pascal Tabu Ley, ambaye pia akijulikana kwa jina la "Rochereau"alizaliwa Novemba 13, 1937 katika kijiji kidogo cha jimbo la Bandundu nchini Kongo. Alijipatia umaarufu wa kuwa nyota wa muziki wa mtindo wa rumba katika miaka ya 1960.
Kutokana na nyimbo zake kama "Adios Thethe" na "Mokolo nakokufa" (siku yangu ya kifo ), Tabu Ley alichangia kuusambaza umaarufu wa mtindo huo na mnamo mwaka 1970 alikuwa mwaafrika wa kwanza kutumbuiza katika ukumbi mashuhuri wa Olympia mjini Paris Ufaransa.
"alikuwa msaniii nguli atika bara zima la Afrika ," alisema Francois Bensignor wa kituo cha muziki cha IRMA mjini Paris..
Pia aliwahi kutajwa na jarida la Jeune Afrique " kama mwanakongo mashuhuri pamoja na aliyekua Rais Mobutu Sese Seko watakaokumbukwa katika historia ya Congo..
Nyumbani , Tabu Ley hakuwa tu mwanamuziki lakini pia alijitosa katika siasa.
Aliteuliwa kuwa waziri wa utamaduni wakati wa utawala wa hayati Rais Laurent-Desire Kabila -- baba wa Rais wa sasa Joseph Kabila, na hatimaye akawa makamu gavana wa Kinshasa.
Alilazimika kuishi uhamishoni wakati wa enzi ya Mobutu Sese Seko(1965 hadi 1997), na mnamo mwaka 1990, utawala huo wa mabavu ulipiga marufuku albam yake "Trop, c'est trop" ( Too much is too much).
0 comments:
Post a Comment