Waziri Mkuu wa Somalia Abdi Farah Shirdon
Bunge la Somalia limeanza kujadili hoja ya kutokuwa
na imani na Waziri Mkuu wa nchi hiyo Abdi Farah Shirdon ambaye amekuwa
haelewani na rais wa nchi hiyo Hassan Sheikh Mahamud.
Wafuasi wa rais Hassan wanasema Waziri Mkuu huyo ameshindwa kutekeleza majukumu yake na uongozi wake umekuwa hauna mafanikio.
Waandishi wa habari waliyopo Somalia wanasema mgawanyiko katika serikali ya Somalia iliyoundwa mwaka jana, unatishia juhudi za kuimarisha utulivu nchini humo baada ya nchi hiyo kuathirika na mgogoro kwa takrabani miongo miwili.
0 comments:
Post a Comment