Katika shamrashamra za kusheherekea sikukuu za Krismasi
pamoja na mwaka mpya, kanisa la Christ Embassy Church leo limetoa zawadi pamoja
na chakula cha mchana kwa watoto yatima wa SOS waishio Dar es salaam, pembezoni
kabisa mwa jengo la Mawasiliano Tower.
Mandhari nzuri ya kituo hicho cha SOS.
Watoto yatima wa SOS wakifurahia michezo.
Akielezea tukio hilo lililofanyika mchana huu kituoni hapo, Mchungaji Ken Igini wa Kanisa hilo la Christ Embassy kwa hapa Tanzania, amesema kuwa wazo hilo la kushiriki chakula cha mchana na watoto hao waliyo yatima, pamoja na kuwapatia zawadi, limetolewa na Rais wa kanisa hilo lililo na makao yake makuu nchini Nigeria, Mchungaji Chris.
Mchungaji Ken Igini.
Aidha katika hatua nyingine Afisa utawala wa SOS Bi Rahma Michael amesema kuwa wamefurahishwa sana na kitendo hicho, huku watoto nao wakieleza kuwa wamefarijika sana na ujio wa kanisa hilo hususani katika kipindi hiki cha sikukuu, ambacho watoto wengine wengi hufurahia msimu huu wakiwa na familia zao.
Afisa utawala wa kituo cha SOS.
Baadhi ya zawadi na vyakula hivyo vilivyotolewa na Christ Embassy Church.
watoto wakifurahia chakula kizuri kilichoandaliwa na Christ Embassy Church.
0 comments:
Post a Comment