Kusini mwa
Afrika: South Africa leo imepata pigo kubwa la kumpoteza mtetezi wa watu
weusi na mpinga ubaguzi wa rangi ndani ya taifa hilo lenye utajiri
barani Afrika, Nelson Mandela, aliyewahi kuvunja rekodi ya kuwa Rais wa
kwanza mweusi nchini humo.
Yeye alizaliwa mwaka 1918 na kufariki jana saa mbili usiku, tarehe 5 Nov mwaka huu (2013)
Mandela aliyewahi kufungwa jela kwa miaka ishirini saba wakati wa enzi za mkoloni ndani ya taifa hilo, alishawahi pia kuwa bondia na mwanariadha huku akiongoza harakati za kumkomboa Muafrika katika utawala wa mkoloni jambo ambalo kwa hakika liliwakera sana Wazungu kwa wakati huo.
Yeye atakumbukwa kwa mengi lakini zaidi ni upendo aliyokuwa nao kiasi cha kukubali kuteswa na kufungwa jela kwaajili ya Waafrika waliyoko kusini mwa Afrika.
Bwana ametoa, bwana ametwaaa... Jina la bwana libarikiwe.
0 comments:
Post a Comment