Kutokana na kuvunjika kwa daraja linalounganisha mji wa Morogoro na Dodoma baada ya mvua kubwa iliyoleta mafuriko hivi majuzi, sasa nyama ya ng'ombe imekuwa ni kitendawili kikubwa katika jiji la Dar es salaam, ukizingatia kuwa jiji hili hutegemea sana kupata kitoweo hicho kutoka mkoani Dodoma.
Hali hii ya utata imelalamikiwa sana na wafanyabiashara wa nyama hapa jijini kutokana na kupandishwa kwa bei ya kitoweo hicho, ambayo mpaka sasa imefikia shilingi 6,000 kwa kilo inayouzwa machinjioni, bei ambayo ni ghali mno, ukilinganisha na siku chache kabla ya kuvunjika kwa daraja hilo.
Aidha kwa upande wa watumiaji wa mboga hii, sasa wamelazimika kununua mboga nyingine kama samaki, maini ama mboga zenye jamii ya kunde kutokana na kukosekana kwa kitoweo hicho kwenye maduka husika, ama kuwa juu kigharama.
0 comments:
Post a Comment