Decoration & Catering Services

Decoration & Catering Services

Boutique

Boutique

Friday, March 28, 2014

Wadau wang'aka mahusiano ya Johari na Ostaz Juma Namusoma.


Nyepesi nyepesi zinazo endelea mitandaoni ni kwamba penzi la mwanadada Johari anaefanya vyema katika filamu, na Ostaz Juma Namusoma, kwasasa linazidi kushamiri ili hali wadau mbalimbali wa tasnia hii ya muziki na filamu, kuonyesha hali ya kutoridhishwa na mahusiano hayo.
Kwa mujibu wa mitandao mbalimbali Ostaz alifunga safari kwenda nchini Afrika Kusini kwa mapumziko mafupi lakini pia kumnunulia mpenzi wake huyo zawadi mbalimbali kwa lengo la kupalilia uchumba wao.
“Jamaa alikuwa Sauzi (Afika Kusini), aliondoka hapa tarehe 17 (Machi) na amerudi tarehe 21. Kamletea zawadi kibao lakini kubwa zaidi ni kamera kubwa, nzuri ya kisasa kwa ajili ya kerekodia filamu,” kilipasha chanzo hicho.
BongoFrag ilifanikiwa kumpata Ostaz kwa njia ya simu, akafafanua: “Ni kweli nilikuwa Afrika Kusini. Kuhusu Johari, ni kweli si mke wangu? Nimemletea zawadi nyingi sana, achana na hiyo kamera unayosema.
“Lengo ni kuweka uchumba wangu  na yeye sawa. Nilitamani sana kusafiri naye lakini sikutaka kufanya hivyo ili kuweka usawa, mke wangu asione nimeegemea zaidi kwa mke mdogo.”
Alipoulizwa kwa nini amemuita Johari mkewe, haraka alisema: “Ndoa ipo karibu, nimeshaamua Johari awe mke wangu wa pili. Wadau wasubiri waone, uzuri ni kwamba dini yangu si kikwazo.”


Je, wadau wanasemaje?


 

0 comments:

Post a Comment