Decoration & Catering Services

Decoration & Catering Services

Boutique

Boutique

Tuesday, April 22, 2014

Tamasha la pasaka Dar lafana kuliko la Morogoro.

 Edison Mwasabwite

Jessica BM na bendi yake.

Glorious Worship Team

Upendo Nkone

Blogger wako nikapata nafasi ya kupiga picha na Keke, saa chache kabla ya yeye kupanda jukwaani.

Keke akauwasha moto

Wacha weeeh!

Hapa Blogger wako uzalendo ulinishinda, nikaingia ulingoni, kazi ikawa pembeni tena. Hatari!

Akiimba kwa ujasiri mbele ya WaTz

Hatariiii!

Tukaipepea bendera ya Yesu kwa ki-Zulu.

Kama ulikosa kuhudhuria Tamasha hili la Pasaka 2014 pale Uwanja wa Taifa, nikupe pole tu kwani vilitokea vitu vingi vizuri mno, huku Mungu akionekana waziwazi kwa kila aliyepanda kutumika katika stage kubwa, iliyoandaliwa na Msama Promotion.

Waimbaji mbalimbali walilipamba Tamasha hili, kama Edison Mwasabwite, Upendo Kilahilo, Upendo Nkone, Masanja, Rose Muhando na wengine wengi, huku funga kazi akiwa ni mwimbaji mahiri na mwenye kila aina ya madoido katika uchezaji wake, Keke kutoka South Afrika.

Aidha kwa mwaka huu Tamasha hili kwa hapa Dar lilifana sana, tofauti na yale ya awali yaliyokuwa na matatizo kedekede kama ubovu wa muziki (sound) n.k.

Hata hivyo siku ya Jumatatu yaani jana, tamasha hili lilipelekwa kule mji kasoro bahari; Morogoro, ambapo tunaelezwa kuwa huko hali haikuwa shwari. Mvua kubwa na tatizo la muziki ndiyo yaliyo lisababishia tamasha hili kuanza saa kumi jioni, tofauti kabisa na ratiba iliyo wekwa, huku wanamuziki wakinyeshewa na mvua mno.

Msama Promotion ndiyo kampuni ya kwanza hapa nchini, kuwaleta wanamuziki mbalimbali wa muziki wa Injili kutoka sehemu tofauti tofauti Afrika yote kama Rebecca Malope, Solomoni Mkubwa, Sara K, Ephraim Sekeleti na Solly Mahalu.

0 comments:

Post a Comment