Katika pitapita zangu za hapa mjini, jana nikakutana na
rappa wa Kibongo aliyekuwa akichipukia vyema sana katika muziki huu wa Bongo
Fleva, Baghdad wa Mexicana Lakavela.
Mimi nilibahatika kumjua kijana huyu
hata kabla ya kuvuma sana kwenye game, tulipokuwa twasoma nae shule moja, pale
Azania Secondary school 2007-2009, mimi nikiwa natumia lebo ya bluu nae
nyekundu.
Sasa kilichonisukuma mpaka saa hii nimeamua kuipandisha stori yake kwenye mtandao huu; ni mabadiliko makubwa sana ya kimuonekano na kiafya ya Baghdad, ambae pia alikuwa ni mahiri sana kwa kucheza Basketball shuleni kwetu.
Sasa kilichonisukuma mpaka saa hii nimeamua kuipandisha stori yake kwenye mtandao huu; ni mabadiliko makubwa sana ya kimuonekano na kiafya ya Baghdad, ambae pia alikuwa ni mahiri sana kwa kucheza Basketball shuleni kwetu.
Katika moja ya pozi akiwa na afya yake ya awali.
Sio siri kijana huyu amebadilika sana, mpaka ninaogopa kila
niikumbukapo picha yake ya Azania na hii ya jana niliyomuona tena live baada ya miaka minne.
Hiyo jana sasa nilipokutana nae nilimsalimia kama mtu nisiye
mjua ila kwa ukarimu na nilipo jaribu
kumuuliza mambo fulani fulani ya huko nilikokuwa naenda, aliniambia ndiko pia
aendako na tena ni Mwenyeji. Na kwa bahati nzuri sana akaniambia kuwa sura
yangu si ngeni kwake.
Kwa upande wangu nilifurahi kusikia hivyo huku moyoni
nikijua kile nilichokuwa nakitafuta nitakipata kiurahisi maana nishampata mtu
anaenifahamu.
Baghdad akiwa kwa stage.
Baada ya hatua chache mbele bro wangu huyu wa xul akaamua
kujitambulisha kuwa yeye ni Baghdad. Ebwana siyo siri nilishtuka sana na
kumuuliza yeye ni Baghdad yupi wa Azaboy au yupi na mbona kakonda sana?( Mungu
anisamehe tu). Ndipo rappa huyu alipo
nijibu kuwa ndiye huyo huyo wa Azaboy na kuwa ni mazoezi tu ndiyo yaliyo
mpunguza.
Lakini hakuonekana kuwa na ujasiri tena, akaamua kuniacha mapokezi.
Ninachotaka kukijua toka kwenu fans wake katika muziki huu
Hip hop, marafiki, ndugu na wale wote mlio karibu nae mwanamuziki huyu Je, ni kweli
mshikaji anapiga mazoezi kiasi cha kupungua vile, au ana tatizo gani linalo
msumbua kiasi cha kuwa alivyo sasa?
Hebu tumia muda wako ku-comment hapo chini about this story.
What’s wrong to my brother kwa vile
unavohisi na unavojua!?
0 comments:
Post a Comment