Decoration & Catering Services

Decoration & Catering Services

Boutique

Boutique

Tuesday, April 29, 2014

'Masanja Mkandamizaji' aruhusu 'wizi' wa kazi za wasanii

 

Masanja akifanya huduma ya maombezi mikoani.

Masanja Mkandamizaji a.k.a Mchungaji mtarajiwa, kwasasa yupo njiani kufyetua albamu yake ya pili baada ya ile albamu yake ya kwanza ya Hakuna Jipya, iliyofanya vizuri sana sokoni.

Akihojiwa na redio moja hapa nchini, Emannuel Mgaya alisema kuwa kwasasa amekwisha maliza tengeneza albamu yake ya pili, ambapo kwenye mahojiano hayo alitoa ahadi kwa wapenzi wa muziki wake, kuwa albamu hii ya sasa itakuwa njema zaidi na itawabariki wengi kwani hata yeye kila aisikilizapo, hubarikiwa nayo.

Lakini kali aliyoitoa mwimbaji huyu wa muziki wa Injili ambae wengi tunamfahamu kama Mchekeshaji, ni kwamba ametangaza kuwa; punde albamu yake itakapo ingia sokoni tu, basi wale wezi wa kazi za wasanii, wanao toa kopi za albamu za watu, waifanye kazi hiyo kwa nguvu sana kwani yeye hatokwazika wala wakamata. Na alipoulizwa sababu ni nini ya yeye kuruhusu kitu hicho, alisema kuwa ni kwasababu anahitaji Injili isonge mbele na iwafikie watu wote hata wa vijijini kwa urahisi na kwa bei poa kabisa.

0 comments:

Post a Comment