Nguli wa muziki wa Raggae hapa nchini, Innocent Ngayagwa alimaarufu kama 'Ras Inno', kwasasa amekwisha panga jeshi la wasanii wa aina za muziki tofauti tofauti, watakao kuwa chini ya kampuni yake inayokwenda kwa jina la Raggae Production House (RPH).
Akizungumza na mmoja kati ya waandishi wetu, Ras Inno alisema kuwa lengo la yeye kufanya shughuli za usimamizi wa kazi za wasanii ni kutaka kuwainua kimuziki na kimaisha, lakini zaidi ni kutaka kuwafundisha ma-meneja, jinsi ya kuwa-meneji wanamuziki.
'Unajua kwa hapa nchini, mpaka sasa sijaona watu wanaoweza kuwasimamia wasanii vilivyo hata wakatoka na wakawa na maisha mazuri kama ilivyo ughaibuni, lah kama wapo basi ni wachache sana' alisema Ras Inno.
Aidha mwanamuziki huyu toka kule Iringa, alisema kuwa mpaka sasa amekwisha waandaa wanamuziki watano; ambao kati yao wapo wanaofanya zouk, mchiriku, rumba, gospel na raggae.
'RPH japo inaanzwa na neno Raggae, lakini haijajikita kwa asilimia zote kwenye muziki huo tu, bali kwa asilimia 50 na asilimia 30 ni kwa aina nyingine za muziki na 20 kwa kazi nyingine kama kuandaa matamasha n.k.' alisema Ras Inno.
Moja kati ya wasanii waliopo chini ya kampuni hii ni Kidawa Abdul Kondo a.k.a Lady - K, ambae kazi yake ya kwanza kama solo artist 'mimi ni wake' imeanza kufanya vyema katika redio mbalimbali hapa nchini. Lady - K amekwisha wahi kuimba katika bendi nyingi kama Mchinga Generation, Tabora Jazz Band na Top Band aliyokuwa akiimba na Alawi Junior na Omary Nyembo a.k.a Ommy Dinpozi
0 comments:
Post a Comment