Trafiki feki akiwa amesimama akiwa amevalia sare za trafiki huku ameshikilia jadala lake la kazi.
- ANA CHEO CHA SAJINI,VITABU VYA KOTOZA FAINI
- WANANCHI WATOA USHUHUDA JINSI WANAVYOMFAHAMU
MSEMO wa mjini mipango, umejidhihirisha wazi baada ya
Jeshi la Polisi mkoani Dar es Salaam
kumkamata askari bandia wa kikosi cha usalama barabarani akiwa amevalia sare za
trafiki akiendelea na kazi pasipo kugundulika kwa siku kadhaa kuwa anafanya
uhalifu.
Trafiki
huyo bandia mwenye cheo cha
sajini, (jina halikupatikana) alikamatwa na Polisi akiwa 'kazini' maeneo ya
Tabata Kinyerezi akiwa amevaa sare mpya ya Askari wa Usalama Barabarani, kikoti
cha kuakisi mwanga na kofia nyeupe.
Pia trafiki huyo alikuwa na
jalada pamoja na kitabu cha kutoza faini (Notification) kwa madereva
wanaopatikana na makosa ya kukiuka sheria za usalama barabarani.
Gazeti hili lilishuhudia
trafiki huyo feki akiwa amekamatwa na Polisi na kisha kufikishwa Kituo Kikuu
cha Polisi Kati, huku akijifanya amepoteza fahamu.
Mashuhuda waliozungumza na gazeti hili, walisema
wanamfahamu trafiki huyo kwa muda mrefu kiasi kwamba madereva wengi
wanamuogopa, kwani akikamata gari hakuna cha majadiliano kama
ilivyo kwa wengine, bali anawatoza faini moja kwa moja kati ya sh. 20,000 hadi
25,000.
"Yule tunamfahamu kwa uchapaji kazi, alikuwa
hataki rushwa hata kidogo, akikukamata ujue umeumia, lazima akuandikie
'notification'," alisema dereva mmoja anayemfahamu trafiki huyo kwa muda
mrefu.
"Wakati wa foleni alikuwa akisimama barabarani
na kuanza kuyaongoza magari, lakini alipoona imekuwa kubwa zaidi alikuwa
akiondoka kwa kuhofia kujulikana," alisema shuhuda mwingine.
Mkazi mmoja wa jijini Dar es
Salaam anayemfahamu trafiki huyo, alisema; "Namfahamu huyu
jamaa mambo yake ni mazuri sana
nyumbani kwake, hivi sio trafiki... ahaaa haiwezekani bwana."
Aliongeza kuwa; "Yule trafiki huwa anatanua sana kwenye baa na kama
kulikuwa na ugeni wa viongozi hasa wa nje alikuwa akisema anawahi kwenda
kulala, kwani ataamka mapema kwenda kuongoza misafara."
B a a d h i y a m a d e r e v a wanaomfahamu
trafiki huyo, walisema hawaamini kama kweli
mtu huyo ni trafiki feki kwani wakati mwingine alipokutana na askari wenye vyeo
vidogo chini yake walimsalimia kijeshi.
Mashuhuda hao walisema trafiki huyo alikuwa
akifanyakazi kwenye maeneo ya Mkuranga na wakati mwingine alionekana
akiwapangia kazi vijana walio kwenye vikundi vya Polisi Jamii ambao wanasaidia
kuongoza magari. Kwa mujibu wa watoa taarifa hao, vijana wa Polisi Jamii
walipomkamata dereva amekiuka sheria za barabarani, walielekezwa kwa trafiki
huyo ambaye bila mjadala aliwaandikia notification.
Watu waliotoa maoni kuhusu tukio hilo, walilihusisha na uzembe katika Jeshi la
Polisi kiasi cha kushindwa kujitambua. "Hawa wenzetu Jeshi la Polisi
hawajajitambua, haiwezekani watu washindwe kutambuana wakati wanafanyakazi
pamoja na mtu huyo," alisema John Edward.
Lakini pamoja na kulishutumu Jeshi la Polisi,
baadhi ya watu walionekana kufurahishwa na kitendo cha trafiki huyo feki
wakisema ni mbunifu wa ajira.
"Ingawa amefanya makosa kwangu mimi naona ni mbunifu wa ajira na amelisaidia sana jeshi la Polisi kwani walikuwa wanakaribia eneo lake la kazi madereva walikuwa waangalifu sana ili kuepuka kupigwa notification," alisema Edwar
0 comments:
Post a Comment