Decoration & Catering Services

Decoration & Catering Services

Boutique

Boutique

Thursday, August 15, 2013

SHEKHE PONDA ASOMEWA MASHTAKA KITANDANI WODINI


Shekhe ponda akiwa hospitalini.


KATIBU wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania, Ponda Issa Ponda, amesomewa mashtaka yanayomkabili chini ya ulinzi mkali wa Polisi wodini katika Taasisi ya Tiba ya Mifupa (MOI).Ponda alisomewa mashtaka yanayomkabili jana jioni mbele ya Hakimu wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Hellen Liwa na Mwendesha Mashtaka wa Polisi, Tumaini Kweka
.Ilidaiwa na upande wa mashtaka kuwa mshtakiwa huyo, Shekhe Ponda, anakabiliwa na mashtaka mawili aliyotenda Juni 2 na Agosti 11, mwaka huu sehemu mbalimbali.Ilidaiwa kuwa Shekhe Ponda alichochea vurugu sehemu mbalimbali za Tanzania. Ilidaiwa kuwa Shekhe Ponda, Agosti 11, mwaka huu alihamasisha vurugu. Pia inadaiwa kuwa Juni 2, mwaka huu Ponda alishiriki tena kuhamasisha vurugu.
 
Sehekhe Ponda alikana mashtaka hayo na kesi hiyo iliahirishwa hadi Agosti 28, mwaka huu, ambapo mshtakiwa ataendelea kuwepo hospitali kwa ajili ya matibabu.Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kusomwa kwa mashtaka hayo, Wakili wa Shekhe Ponda, Juma Nassoro, alisema hati hiyo ina makosa kwani Agosti 11, mwaka huu siku ambayo anadaiwa kutenda kosa hilo, alikuwa tayari amelazwa hospitalini, hivyo wataleta pingamizi la kufuta kesi hiyo itakapotajwa. 
 
Alisema leo walikubaliana a f a n y iwe ma h o j i a n o kwa kumtuhumu kufanya uchochezi maeneo ya Zanzibar, Dar es Salaam na Morogoro."Tulipinga yasifanyike mahojiano hayo kwa kuwa Shekhe Ponda ameishawasilisha malalamiko yake Ofisi za Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora kutokana na polisi kudai kuwa hawajampiga risasi Shekhe Ponda," alisema wakili huyo. Pia alisema Ponda ameishapeleka malalamiko yake Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi. 
 
Aliongeza kwamba mahojiano hayo hayakufanyika kutokana na hali ya Shekhe Ponda kutokuwa nzuri. "Lakini baada ya saa tatu wamemsomea mashtaka kuanzia saa 10 jioni," alisema.Nje ya MOI ulinzi uliimarishwa na hakuna mtu aliyeruhusiwa kuingia wodini kuangalia wagonjwa kwenye block aliyolazwa Shekhe Ponda. 
 
Magari ya Polisi yasiyopungua manne yalikuwa yameegeshwa eneo hilo yakiwa na askari polisi waliojidhatiti kwa silaha.Wafuasi wa Shekhe Ponda walisikika wakilalamika baada ya kuzuiwa kuingia wodini kumuona na kuhoji; "Kila sehemu mnatuzuia, tunahitaji kumuona Shekhe

0 comments:

Post a Comment