Decoration & Catering Services

Decoration & Catering Services

Boutique

Boutique

Tuesday, November 26, 2013

Mrisho Mpoto alizwa na Ismail





 Mpoto na Ismail

Katika hali ya kusikitisha kwa wale wapenzi wa Mpoto Band, leo blog hii ilipata nafasi ya kuzungumza na Mrisho Mpoto juu ya maendeleo ya bendi yake inayotamba sana hapa nchini haswa kwenye matukio muhimu ya kijamii na kiserikali, na kubaini kuwa Ismail hayupo tena kwenye band hiyo.

Katika kulifafanua hilo, Mpoto alisema kuwa Ismail ameondoka kwenye band hiyo kutokana na mambo fulani yaliyowafanya wasielewane na kumsababisha Ismail kukasirika na kuondoka.

"aaah Ismail hayupo siku hizi kwenye band, ila ni hasira tu naamini atarudi kwani mambo kama haya hutokea katika tasnia"

Ismail nae amekiri kuwa hayupo kwenye band hiyo kwasababu fulani za kimaslai, alizogoma kuziweka wazi.

0 comments:

Post a Comment