Decoration & Catering Services

Decoration & Catering Services

Boutique

Boutique

Wednesday, November 27, 2013

Viongozi wa kisiasa Ujerumani wakubaliana.


Viongozi wa vyama vya kisiasa nchini Ujerumani vya Christian Social Union-CSU, Christian Democratic Union-CDU na Social Democratic, SPD, wamekubaliana juu ya masharti ya kuunda serikali ya mseto. Baada ya kikao cha mwisho cha majadiliano kilichodumu kwa saa 17, vyama hivyo vimekubaliana kuwaruhusu watoto wanaozaliwa nchini Ujerumani na wazazi wanaotoka nchi za nje, wapewe pasi mbili za kusafiria, kwa masharti fulani. Pia wamekubaliana kuanzisha kima cha chini kitaifa cha mshahara cha Euro 8 na senti 50 kwa saa kuanzia mwaka 2015. Makubaliano hayo yaliyofikiwa yanakamilisha mazungumzo ya kuunda serikali yaliyodumu kwa miezi miwili.

0 comments:

Post a Comment