Decoration & Catering Services

Decoration & Catering Services

Boutique

Boutique

Monday, December 30, 2013

KIMATAIFA: Askari wawili wa kulinda amani Sudani wauwawa.

Askari UN

Askari wawili wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan, wameripotiwa kuuawa katika jimbo la Darfur nchini humo. 

Askari hao wametajwa kuwa ni raia wa Senegal. Kwa mujibu wa habari, askari hao wa kulinda amani waliuawa jana baada ya kushambuliwa na watu wenye silaha ambao hadi sasa bado hawajajulikana. 

Mbali na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kulaani hatua hiyo, amekitaja kitendo hicho kuwa kisichofaa na kuitaka serikali ya nchi hiyo kuhakikisha inawatia mbaroni wahusika wake na kuwafikisha katika vyombo vya sheria haraka iwezekanavyo.

Tangu mwaka 2003 ambapo makabila yalisimama kupambana na serikali ya Khartoum kupinga kile yalichokiita kuwa, ni ubaguzi wa rangi dhidi yao, sheria zimekuwa zikikanyagwa katika baadhi ya maeneo ya jimbo hilo la Darfur. 

Kufuatia hali hiyo, mwaka 2007 vikosi vya Umoja wa Afrika na vile vya Umoja wa Mataifa UNAMID vilitumwa jimboni hapo kwa lengo la kukakibiliana na makundi ya wabeba silaha. Hii ni katika hali ambayo hadi sasa jumla ya askari elfu 14 na 500 polisi elfu nne wanasimamia usalama katika jimbo hilo.

Chanzo: BBC Swahili.

0 comments:

Post a Comment