Pichani: Mmoja wa wananchi wa Taifa hilo, katika moja ya mandamano.Watu 18 wameuawa tangu kutokea milipuko mjini Cairo siku ya Ijumaa.
Vikosi vya usalama vimewekwa katika hali ya tahadhari wakati ambapo mikutano miwili ya makundi hasimu nchini Misri ikitarajiwa kufanyika ili kuadhimisha miaka mitatau ya kuondolewa madarakati kwa rais wa zamani Hosni Mubarak.
Wafuasi wa aliyekuwa rais wa taifa hilo Mohammed Morsi pamoja na wale wa serikali inayoungwa mkono na jeshi wanatarajiwa kufanya maandamano katika miji mikubwa nchini humo.
Vuguvugu la Muslim Brotherhood limeshutumu milipuko hiyo lakini wapinzani wake wamelikosoa kundi kwa kuendeleza mashambulizi kama hayo.Hali ya wasiwasi iliongezeka hapo jana baada ya misururu ya milipuko ya mabomu na ghasia katika maeneo tofauti nchini humo ambayo imesababisha vifo vya watu 18 huku wengine wakijeruhiwa.
Inaarifia wapiganaji wamezidisha mashambulizi dhidi ya utawala wa Misri, huku milipuko kadhaa ikisikika katika mji mkuu Cairo
Mashambulizi hayo yanatokea katika mkesha wa kuadhimisha mwaka wa tatu tangu kuondolewa mamlakani kwa aliyekuwa Rais Hosni Mubarak.
Chanzo: BBC
0 comments:
Post a Comment