Pichani: Mustafa Hassanali.
Katika muendelezo wa sherehe za Muungano wa Tanganyika na Zanzibar uliozaa nchi ijulikanayo kama Tanzania miaka 50 iliyopita, Ubalozi wa Tanzania huko Urusi, umemualika mbunifu mahiri wa mavazi Mustafa Hassanali kutoka hapa nchini, kufanya onesho la mavazi yake katika siku hiyo ya Muungano ya tarehe 26 Aprili, huko jijini Moscow.
Hassanali ambae mpaka sasa amekwisha kufanya maonesho ya
namna hiyo kwenye miji 26 katika nchi 17, onesho hili lililo na jina MUUNGANO, litamtimizia
mbunifu huyu jumla ya idadi ya miji 27 na
nchi 18 alizowahi fanya maonesho ya mavazi.
Aidha mbali na kufurahishwa sana na mualiko huo, Mustafa
Hassanali amesema kuwa katika onesho hilo atatumia rangi ya ugoro na Khanga,
kunakshia mavazi mbalimbali ya siku hiyo itakayo hudhuriwa na wafanyabiashara Wakitanzania
na watu wenye asili ya Afrika waishio huko Urusi.
Hili litakuwa ni onesho la tatu kufanyika barani Ulaya, baada
ya yale ya Uitaliano na Sweden, ambapo kwa mwaka 2011 Mbunifu huyu alialikwa katika Ubalozi wa
Sweden, jijini Stockholm kusheherekea miaka
50 ya Uhuru wa Tanganyika, akiwa kama mbunifu kutoka nje
.
0 comments:
Post a Comment